Huu Ni Utumwa Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuuepuka


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu

Kama kuna maisha magumu ambayo mtu anaweza kuyachagua ni kuchagua kuwa mtumwa na kuishi maisha ambayo huyafurahii hata kidogo.
Upo utumwa wa aina nyingi sana ila kwa leo ningependa kuzungumzia utumwa huu wa kuwa na chanzo kimoja cha kipato. Ndio utumwa wa chanzo kimoja cha kipato.
Chanzo kimoja ni hatari sana hasa pale chanzo kile kinapokuwa ni ajira. Itakufanya kuwa mtumwa.

Mwingine atasema haiwezekani?
Ebu ngoja tuone chanzo kimoja kinavyoweza kukufanya kuwa mtumwa
1. Itakufanya usiwe na uhuru wa kutoa maoni yako na kukemea uovu wowote ambao utaona unajitokeza kwa sababu tu usije ukapoteza kazi yako.
2. Unafanya kazi muda mwingi unalipwa kidogo.
Unatumia muda mwingi kazini kwa siku unatumia masaa nane au zaidi kwa ajili ya kufanya kazi na mshahara  unalipwa kidogo
Yaani wewe unashughulika unafanya kazi na kumwingizia  kipato asilimia 100℅ na unalipwa asilimia 1% na asilimia 99% ni ya kwake.

3. Unalipwa mara kumi na mbili kwa mwaka.

hili ni jambo nimekuwa nawaambia watu wengi sana kwamba kwamba wewe umesoma kwa miaka kumi na tano na zaidi. Umeajiriwa kwenye kampuni ambayo inakulipa vizuri na unalipwa mara kumi na mbili kwa mwaka. Ndio mara kumi na mbili. Wakati kampuni inaingiza PESA kila siku. Yaani kwa mwaka inaiingiza pesa mara 365. Sasa wewe ni lini unategemea kuja kufikia hapo.
4. Mshahara wako unakatwa hata kabla hujauona. Wakati wewe unajitahidi kufanya kazi kwa bidii kubwa sana na mwishoni mwa mwezi pesa ya mshahara kabla ya wewe hujaiona inakatwa kodi bila ya wewe kuigusa kwanza.
Wakati ukiwa na biashara yako pesa yako unaweza kuamua ni lini ikulipe iwe kwa siku wiki au mwezi.
5. Sio biashara yako.
Mwandishi wa kitabu cha HOW TO BECOME RICH IN SEVEN STEPS Robert Kiyosaki
Anasema “Mind your own Business” Jali biashara yako.
Akiwa anamaanisha  kwamba hauitaji kuutumia muda wote kwenye kufanya kazi za wengine bali tenga muda kidogo kwa siku ambapo utaweza kushughulika na biashara yako.  Mwandishi unapofa
unapofanya kazi kwenye kampuni ya mtu mwingine unakuwa hujali biashara yako bali unajali biashara za watu wengine. Igundulike kwamba kuajiriwa sio kitu kibaya hata kidogo, ajira ni daraja lako binafsi katika kuelelekea uhuru wako wa kiuchumi. Ajira ni chanzo cha kwako kufanikiwa na kufanya buashara zako kwa ufanisi
bali ni chanzo kizuri cha kuanzia biashara.
Nifanyeje sasa?
Amua sasa wakati ni sasa muda ni sasa na badilika sasa
Amua sasa kuanza kuanzisha kitu ambacho kinakuingizia pesa kwenye mfuko wako na kifanye kwa umakini jiondoe kwenye utumwa huu maana kila kitu kinawezekana na kutu cha kitakachokusaidia ni wazo lako zuri la kibiashara. Wazo bila matendo halina maana. Liweke katika matendo sasa wazo lako. Katika kuanza ndipo utakapokutana na changamoto na kukabiliana nazo.

Weka mmalengo ambayo utayafanyia kazi.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.


4 responses to “Huu Ni Utumwa Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuuepuka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X