-
Jinsi ya kuchagua Watu Sahihi na Vitabu Sahihi Kwa Maendeleo Yako Ya Miaka Mitano Ijayo
Katika makala ya jana rafiki yangu. Niliandika Siri ya Mabadiliko ya Kweli. Miaka Mitano Ijayo Utakuwa Jinsi Ulivyo Isipokuwa Kwa Vitu Hivi Viwili. Baada ya kuelewa kuwa watu unaokutana nao na vitabu unavyosoma vina mchango mkubwa katika kukufanya mtu tofauti baada ya miaka mitano, swali linalofuata ni: unawachaguaje watu sahihi? Na unachaguaje vitabu vitakavyokujenga kweli?
Hii si kazi ya kubahatisha. Ni mchakato unaohitaji umakini, nidhamu, na maamuzi ya makusudi. Makala hii inakuonyesha njia ya kuchagua vyanzo hivi viwili vya mabadiliko ili kuimarisha safari yako ya mafanikio.
1. Jinsi ya Kutambua Watu Sahihi wa Kukua Nao
Kila mtu anayekuzunguka ana athari katika namna unavyofikiri na kutenda. Ili ukue:
a) Tafuta Watu Wenye Maono na Nidhamu
Watu wanaojitambua na wenye mwelekeo wa maisha hukupa msukumo wa kufanya makubwa. Hawapotezi muda kwenye manung’uniko au visingizio. tafuta watu wa namna hii rafiki yangu.
b) Watafute Waliofika Unakotamani Kufika
Kama kuna watu wamefikia mafanikio na hatu ambayo wewe unatamani kuwa umefikia, hawa ni washauri wa kweli. Wanaweza kuwa wafanyabiashara waliobobea, viongozi wa kiroho, au hata walimu wa kawaida lakini wenye hekima ya maisha. Ukiwapata watu wa namna hii kamwe usiwaachie, washikilie na uende nao ili wakusaidie kuweza kufikia ndoto zako kubwa.
c) Jihadhari na Watu Wanaopunguza Ndoto Zako
Wapo watu ambao kila mara huona sababu ya kwa nini jambo haliwezekani. wanadogosha lengo lako na ndoto zako. Wanaeneza hofu na mashaka. Epuka kuwaruhusu wawe sauti kuu katika maisha yako. Kumbuka kwamba ukikaa na waridi lazima utanukia. Sasa kazi ni kwako kuhakikisha kwamba unachagua waridi linalokufaa. La sivyo yeyote utakayechagua atakuwa sehemu ya maisha yako.
d) Jiunge na Mitandao ya Ukuaji
Kuna vikundi vya watu wanaojifunza pamoja – iwe ni vikundi vya kusoma, vya maadili ya kazi, au vya ujasiriamali. Huko ndiko mahali pa kukutana na watu sahihi.
2. Mambo ya Kuzingatia Katika Kuchagua Vitabu vya Kujenga Maisha Yako
Vitabu ni marafiki wasiochoka kukuinua. Lakini si kila kitabu kinajenga. Ili upate thamani:
a) Soma Vitabu Vinavyoendana na Malengo Yako
Kama lengo lako ni kuimarika kifedha, soma vitabu vya fedha. Kama unataka kuimarika kiroho, tafuta vitabu vya kiroho. Usisome tu kwa sababu “kila mtu anasoma.” Kumbuka vitabu vipo vingi na siyo vitabu vyote vinakufaa wewe. Kitabu ambacho kinasomwa na mwingine kinaweza kisiwe kizuri kwako, ndiyo maana wewe mwenyewe unapaswa kuwa mtu wa kuchagua kwenye hili suala.
b) Angalia Waandishi Wenye Matokeo Yanayoonekana
Soma vitabu vilivyoandikwa na watu walioishi kile wanachofundisha. Mfano: Mwandishi wa kitabu cha biashara ambaye ana biashara hai, au mshauri wa ndoa mwenye ndoa yenye afya.
c) Usipuuze Vitabu vya WASIFU NA TAWAFIFU (Biographies)
Kusoma maisha ya watu waliopitia magumu na kufanikiwa hukufundisha hekima ya kipekee isiyopatikana darasani. Wasifu wa watu kama Nelson Mandela, Wangari Maathai, Steve Jobs au Elon Musk unaweza kuwa chachu ya mafanikio yako. Hakikisha vitabu vya namna hii unakuwa navyo vingi na uvisome mara kwa mara. Anza na hiki hapa chini kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391 au 0684408755 sasa
d) Kuwa na Mpango wa Kusoma
Chagua angalau kitabu kimoja kwa mwezi, ukigawanya kwenye ratiba ya kila siku. Ni bora usome kurasa 10 kwa siku kwa nidhamu, kuliko kusoma kurasa 100 mara moja kisha ukaacha. Ukiweza kusoma kurasa kumi kila siku kwa mwezi utakuwa umeweza kusoma kurasa 300 kwa mwezi. Hii ndiyo kusema kwamba kila mwezi utakuwa unaweza kumaliza kitabu kimoja. Kwa mwaka utakuwa umeweza kumaliza vitabu siyo chini ya 12. Kwa hakika utakuwa unaweza kupiga hatua kubw aukilinganisha na asilimia kubwa ya watu ambao huwa hawasomi vitabu.
3. Chukua Hatua Leo: Unda Mazingira ya Mabadiliko
- Fanya orodha ya watu watatu unaopaswa kuwasogelea kwa ajili ya kujifunza kutoka kwao.
- Andika vitabu vitatu unavyotamani kusoma ndani ya miezi mitatu ijayo.
- Anza sasa – usingoje “wakati mzuri.” Mabadiliko huanza pale mtu anapochukua hatua ya kwanza.
Watu sahihi ni daraja la mafanikio yako. Vitabu sahihi ni ramani ya safari yako. Usisubiri miaka mitano ikupite ukiwa bado palepale. Chagua kwa makusudi marafiki wa kukuinua na maarifa ya kukujenga.
Kwa hiyo, swali ni hili:
Leo unamruhusu nani akuathiri, na unasoma nini kila siku?
Je, ungependa mapendekezo ya vitabu bora au njia za kuwapata washauri wa kukuinua? Acha maoni yako au tuandikie kupitia songambele.smb@gmail.com tungependa kusaidia safari yako ya ukuaji.
-
Siri ya Mabadiliko ya Kweli. Miaka Mitano Ijayo Utakuwa Jinsi Ulivyo Isipokuwa Kwa Vitu Hivi Viwili
Katika safari ya maisha, watu wengi hutamani kubadilika, kuboresha maisha yao, na kufikia mafanikio makubwa. Lakini wengi hukata tamaa baada ya miaka kupita bila kuona tofauti kubwa. Swali ni: kwa nini baadhi hubadilika na kupiga hatua, huku wengine wakibaki vilevile?
Msemaji na mwandishi maarufu, Charlie “Tremendous” Jones, alitoa kauli yenye nguvu sana:
“Miaka mitano kuanzia sasa, utakuwa mtu yule yule wa leo isipokuwa kwa watu uliokutana nao na vitabu ulivyosoma.”
Hii si tu kauli nzuri ya motisha ni kanuni ya maisha. Inatufundisha kuwa mabadiliko ya kweli hayatokei kwa bahati, bali kwa maamuzi ya kila siku ya kujifunza na kujizunguka na watu sahihi.
1. Watu Uliokutana Nao: Msingi wa Ukuaji wa Kijamii na Kiakili
Watu tunaowaruhusu kuingia kwenye maisha yetu wanaweza kutuinua au kutuvuta chini. Marafiki, washauri, wakosoaji, na hata wapinzani wote huathiri namna tunavyofikiri, tunavyoongea, na tunavyotenda.
- Kukutana na mtu mwenye maarifa kunaweza kufungua milango ya fursa mpya.
- Mshauri mzuri anaweza kukuokoa na makosa ambayo yangegharimu miaka ya maisha yako.
- Rafiki mbaya anaweza kuchelewesha ndoto zako kwa kukushawishi kushughulika na mambo yasiyo na maana.
Jiulize: Ni watu wa aina gani nimewakaribisha katika maisha yangu? Wananisaidia kukua au wananikandamiza?
2. Vitabu Ulivyosoma: Mbegu za Mabadiliko ya Akili
Kitabu kizuri kinaweza kubadilisha fikra zako milele. Kinaweza kukuamsha toka usingizini wa kiakili na kukuonyesha namna mpya ya kuona dunia. Kusoma ni kama kuzungumza na watu wakuu ambao huenda huna nafasi ya kukutana nao ana kwa ana.
- Kitabu cha kifedha kinaweza kukuonyesha namna ya kutoka kwenye madeni.
- Kitabu cha motisha kinaweza kukuamsha uanze kuchukua hatua ulizokuwa unahofia.
- Kitabu cha maarifa kinaweza kukufanya kuwa mtaalamu katika eneo fulani na kukuongezea kipato.
Jiulize: Ni vitabu gani vimenisaidia hadi sasa? Na ni vitabu gani ninahitaji kuvipitia ili kufikia ndoto zangu?
3. Chukua Hatua: Fanya Uchaguzi wa Kukua
Usingoje miaka mitano ipite bila mabadiliko. Anza leo kwa:
- Kutafuta watu chanya wanaokutia moyo, wanaojua zaidi yako, na wanaotamani kuona unafanikiwa.
- Kujipangia mpango wa kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi. Hata ukianza na kurasa chache kwa siku, utaona matokeo.
Miaka mitano si mbali. Itafika, iwe umebadilika au la. Swali ni: utakuwaje baada ya miaka hiyo? Utakuwa mtu mpya, mwenye fikra kubwa, malengo makubwa, na hatua kubwa au utakuwa bado unalalamikia maisha yale yale?
Jibu liko mikononi mwako. Anza leo kukutana na watu sahihi na kusoma vitabu bora. Hapo ndipo mabadiliko ya kweli huanzia. Na kama unataka kupata vitabu vya kweli vya kubadili maisha yako. Tuwasiliane sasa kupitia 0755 848 391 au 0684408755
Pia nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye channel yetu ya telegram ambapo naweka makala mpya kila siku ambazo unaweza kuzitumia kujifunza na kuchukua hatua. Jiunge na channel yetu hapa.
Je, upo tayari kuwekeza katika mabadiliko yako?
Tuandikie vitabu gani vimekugusa au ni watu gani wamekuwa chachu ya mafanikio yako. Tunapenda kusikia kutoka kwako! Tuandikie kwenye email ya songambele.smb@gmail.comPia usisahau kujiunga na semina yetu ya mwezi huu wa sita ambayo itafundisha mambo mengi kwa undani.
-
Kama haliwezekani kwao, haimaanishi kwamba haliwezekani kwako
Rafiki yangu jambo ambalo watu wengine wanafikiri kwamba haliwezekani kwako siyo kwamba haliwezekani bali linawezeakana. Inawezekana jambo hilo haliwezekani kwao, lakini siyo kwamba haliwezekani kwako. Hivyo, basi zamu ijayo ukisikia mtu anakwambia kwamba jambo hilo haliwezekani, basi jua kwamba linawezekana vizuri tu.
Leo nimekuandallia ebook nzuri sana kuhusu hili suala la kuwezekana. Naomba uisome hapa.
-
Mchakato ni bora zaidi kulliko malengo
Kwenye mojawapo ya kitabu cha Robert Kiyosaki, ameandika kwamba watu wengi huwa wanapambana kuweka malengo ila huwa wanasahau kitu kimoja muhimu sana. na kitu hiki siyo kingine bali ni mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto ambazo mtu unakuwa nazo.
Kumbe moja ya changamoto ambayo inawakumba watu wengi wanaoweka malengo siyo tu kuweka malengo, bali ni kuweka malengo na kutoyafanyia kazi. suluhishio la hili ni kuwa n mchakato kamili wa kufanyia kazi malengo yako mpaka yatimie. Na hapa ndipo unakuja huo usemi unaosema kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko malengo.
Unajua kwa nini watu wengi huwa wanaweka malengo kwa mfano malengo ya kuweka akiba ila bado huwa wanashindawa kuyafanikisha ilihali malengo hayo huwa ni mazuri na ya kupendeza. Ukweli ni kwamba mchakato wa kufanyia kazi malengo hayo ndiyo huwa unakosa.
Kumbe, mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
Unapokuwa na mchakato maana yake, malengo yako unayapa nguvu. malengo yako unawekea mfumo wa kufanyika hata kama haupo. malengo yako unayapa uhai.
Mfano kama lengo lako ni kuweka akiba. unaweka mfumo wa kukata hela kwenye akaunti yako kila inapoingia. au kila baada ya muda fulani. hapo unakuwa umeweka mchakato. na mchakato huu utakuwezesha wewe kufanikisha lengo lako bila wasiwasi wowote. Ndiyo maana nakwambia kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko hata lengo lenyewe unalokuwa nalo.
SASA SWALI la kujiuliza siku ya leo ni kwamba je, una malengo yoyote ambayo umeyaweka kwenye maisha yako. kama una malengo, basi ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unayawekea mchakao wa kuyafanyia kazi haya malengo bila kuacha.
kama utakwama kwenye kuweka mchakato wa kufanyia kazi malengpo yako, basi tunaweza kuwasiliana sasa. Tuwasiliane kupitia barua pepe godiusrweyongeza@gmail.com ili niweze kukusaidia kwenye hilo.
Kumbuka kwamba lengo lolote lile unaloweka, linaweza kuwekekewa mchakato wa kulifanyia kazi. changamoto inakuwa tu pale unapokuwa hujui namna ya kuweka mchakato kwenye lengo lako ili liweze kufanikiwa. lakini fahamu wazi kuwa mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
KUMBUKA Pia kwamba, kama hujui namna ya kuweka mchakato halisi wa kuweka malengo, basi unaweza kuwasiliana nami ili niweze kukusaidia kwenye hili.
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
07555 848 391
Morogoro-Tz
-
Fanya kitu hiki kila siku ili uweze kuishi ndani ya siku yako kwa ushindi mkubwa sana
Kabla ya kuianza siku yako, hakikisha umeipangilia vizuri. Hakikisha unajua kila kitu unachoend akufanya ndani ya siku husika kwa usahihi. HILI LITAKUSAIDIA SANA KUONDOA MWANYA WA WEWE KUFANYA MAMBO AMBAYO SIYO SAHIHI
Kumbuka kwamba unapoipoteza siku moja, unakuwa siyo tu unaipoteza hiyo. unakuwa unapoteza maisha yako. Sasa utapoteza maisha yako mara ngapi? kumbuka muda unaopita leo haurudi tena. Ukienda ndiyo umeenda huo. Ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba muda wote na mara zote unakuwa na ratiba maalum ili kujiepusha na kupoteza muda kwa kufanya vitu ambavyo siyo vya msingi.
Unapokuwa bize kwenye ratiba yako muda wote maana yake unakuwa unaifanya akili yako pia iwe bize. Usipokuwa bize ni sawa na kutimiza ule usemi unaosema kwamba an empty miund is devils workshop.
Hii ndiyo kusema kwamba ukisoma kitabu unajiepusha na majanga mengi.
-
Barua za warren Buffet
Moja kati ya wawekezaji wakubwa sana tulionao kwenye nyakati zetu ni Warren Buffet. Huwa anaandika babrua kila mwaka kwa wawekezaji waliowekeza kwenye kampuni yake ya Berishire Hathaway.Ninaenda kuwa nasoma barua zake zote mmoja baada ya nyingine, kila siku. Nitakuwa nakushurikisha hapa ninachojifunza ili na wewe uweze kujifunza na kufanyia kazi kile unachojifunza.
Endelea kufuatilia mafunzo zaidi hapa bila ya kukosa
Kariobu sana
-
Jinsi Bei ya Kuchapisha Kitabu Inavyopangwa: Mambo Muhimu ya Kuzingatia
Moja ya swali ambao watu wengi huwa wanauliza ni kuwa je, kitabu changu kitagharimu kiasi gani kutoa nakala moja? Jibu la hili swali haliwezi kuwa sawa kwa watu wote. Hii ni kutokana na sababu kadhaa ambazo ndizo huwa zinatoa mwongozo kwenye uchapishaji wa vitabu. Sababu hizi ni pamoja na:
1. Ukubwa wa kitabu. Kitrabu chenye ukubwa wa kurasa 50 hakiwezi kutolewa kwa bei sawa na kitabu chenye kurasa 150 kama vitu vingine vyote viko sawa.
2. Idadi ya nakala unazotoa. Mara nyingi kama unatoa nakala nyingi kuanzia mia tano, bei yake huwa inakuwa chini ukilinganisha na pale unapotoa nakala chache.
3. Rangi na vielelezo. Kama kitabu chako kina vielelezo vya rangi, na kinatakiwa kitolewe kwa rangi bei yake itakuwa juu kidogo ukilinganisha na kitabu ambacho kitatolewa kwa black and white.
4. Mpangilio wa kitabu. Vitabu huwa vinapangiliwa kwenye mifumo tofauti, mfano A4, A5, A6, B5 na mifumo mingine. Hiki ni kitu kingine kitakachoamua bei ya kitabu chako kimoja kinachotolewa iweje. Kitabu cha kurasa 100 cha A5 hakiwezi kuwa na bei sawasawa na kitabu cha kurasa 100 cha A6 hata kama vitu vingine ni sawa kama rangi n.k Kitabu cha A5 bei yake itakuwa ni kubwa kidogo. Wakati huohuo wakati kitabu cha A4 bei yake itakuwa ni kubwa zaidi.
Hivyo ndivyo vitu ambavyo huamua bei ya nakala moja ya kitabu unayotoa iwe na bei kiasi gani.
Kama umeandika kitabu na ungependa kutoa nakala zako. Tuwasiliane nikueleze zaidi ni nini unachotakiwa kufanya ili utoe nakala zako mara moja. Nicheki hapa kwa maelezo zaidi
Kuna raha yake kwenye kutoa nakala ngumu
-
Mfungo
Sizungumzii mwezi wa Ramadhan, wala Kwarezima. Nazungumzia mfungo.
Kwamba kuna kitu ulikuwa unafanya, ila kinakutoka kwenye mstari wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Sasa unaamua kwamba nafuga na ninaacha kukifanya kwa wiki moja.
Kwa mfano ulikuw aunatumia muda mwingi facebook, au youtube au tiktok, unaamua sasa kwa wiki moja ijayo naondoa hii tiktok kwenye simu yangu, na muda ambao nilikuwa nautumia huku ngoja niuweke kwenye kazi.
Yaani, kwamba ile tabia ambayo huipendi, ambayo inakukwamisha unaachana nayo, unajenga tabia mpya, nzuri ya kukufanya usongembele.
Hii unaweza kuifanya hata leo….Usisubiri mwezi wa ramdhan au Kwarezima.
Hivi ndivyo utazidi kuwa bora kwenye maisha yako, hivyo ndivyo utazidi kufanya mazuri na kuwa imara zaidi.
Ni kitu gani ambacho unaenda kufunga kuanzia siku ya leo?
Tujadiliane hapa chini
-
Twende kidijitali mwaka 2025
Rafiki yangu, najua umekuwa unatumia mtandao wa intanenti kwa muda. Lakini kitu ambacho sina uhakika nacho ni kama umekuwa ukiutumia mtandao huu kwa manufaa. Sasa, 2025 twende kidijitali rafiki yangu.
Unajua kwa nini nakwambia hivi, kadiri siku zinavyokwenda, mambo yanazidi kufanyika kidijitali zaidi. Mfano, siku hizi unaweza kuwa nyumbani asubuhi mpaka jioni na mambo yote yakaendelea bila kukwama.
Unaweza kuwa nyumbani na ukafuatilia kila kitu kinachoendelea ofisini kwako kupitia camera ambazo zinapatikana kwa bei nzuri madukani.
Unaweza kuwa nyumbani ukaagiza chakula kikaja mpaka hapohapo.
Unaweza kuwa nyumbani ukatoa au ukaweka hela benki.
Ukawatumia watu hela na mengine mengi.
Unaweza kuwa nyumbani kwako, ukaagiza bidhaa China.
haya yote yanawezekana kwa sababu biashara nyingi zinaenda kidijitali.
sasa cha kujiuliza wakati watu wanaweka biashara zao mtandaoni, wewe biashara yako au kipaji chako kipo huku?
Ndiyo maana, nataka uende kijitali mwaka 2025.
na kwenye hili sina mengi.
nina mabo yafuatayo ambayo kama utayafanyia kazi, yatakuweka mtandaoni moja kwa moja.
moja, fungua tovuti na blog ya biashara yako. Huku weka taarifa za biashara yako, ili iwe rahisi watu wakiingia mtandaoni na kutafuta taarifa za biashara yako wazipate.
Huku weka na bidhaa ulizonazo, na namna watu wanavyoweza kuzipata.
Pili, fungua akaunti kwenye mojawapo ya mtandao wa kijamii. kwakuanzia usianze na kila mtandao wa kijamii, hutaweza. Itakuwa ngumu kwako kuwa instagram, facebook, linkeldn, twitter, tiktok na mitandao mingine ya kijamii. Chagua mtandao mmoja tu. anza na huo. Fungua akaunti huko, na weka maudhui yanaoendana na biashara yako.
hapo sasa umeanza kwenda kidijitali.
Ukishakuwa na wafuasi wa kutosha kwenye mtandao huu, utatanua na kwenda kwenye mitandao mingine.
Kama utahitaji msaada zaidi kuhusu kwenda kijiditali, tunaweza kupanga kufanya mazungumzo ya dakika 15 kati yangu mimi na wewe, ili nikupe ushauri unaoendana na kile ambacho unafanya.
Jibu ujumbe huu kwa kutuma neno KIDIJITALI 2025 ili tupange ratiba ya kuongea.
-
Kufufuka
Kheri ya pasaka rafiki yangu.
Kwa wakristo pasaka, ni kufufuka.
Hata kama wewe siyo mkristo, bado hapa kuna kitu cha kujifunza. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kufufuka.
Nataka na wewe ufufuke.
Kwenye maisha ya kila siku tunaanguka. Tunakumbana na vikwazo vingi ambavyo vinatuzuia kusongambele na kufanya makubwa. Tunaanzisha biashara zinakufa.
Muda mwingine mahusiano yetu yanaptia kwenye changamoto. Hivi vitu VYOTE tunaweza kuvifananisha na kufa.
Sambamba na hayo yote ni kwamba, bado tunapaswa kufufuka bila kujali tunapitia changamoto ngapi. TUFUFUKE.
Kumbuka kwamba, kama tuko hai kwenye maisha yetu, lazima tutakutana na nyakati nyingi za KUFA, ILA BADO TUNAPASWA KUFUFUKA.
TUFUFUKE.
Imeandikwa nami rafiki yako
Godius Rweyongeza