Sababu Tano Kwa Nini Unakutana na Vikwazo na Changamoto


 

Binafsi sio mpenzi wa kuangalia tamthiliya, ila kipindi nipo sekondari nilisoma sana vitabu vya tamthiliya . Kwenye vitabu hivi huwa kuna mhusika mkuu. Mhusika mkuu huwa anakutana na changamoto, kuna wakati anaweza kupigwa kiasi kila mtu akadhani amekata roho, kumbe bado yu hai. Kuna wakati mpaka anaweza kutupwa  kwenye maeneo ya hatari ila baadaye ukashangaa akatoka kwenye hayo  mazingira na kuendelea na safari   wahenga walilijua hili ndiyo maana walisema; Safari ya shujaa haikosi vikwazo.  Kumbe! Kumbe ili uitwe shujaa lazima ukutane na vikwazo kwanza? Kwa Nini vikwazo vinatokea na ufanye nini vikwazo vinapotokea. karibu sana kwenye makala ya leo ambapo nitakueleza kiundani Sababu Tano Kwa Nini Unakutana na Vikwazo na Changamoto na Nini Cha kufanya unapokutana na changamoto.

1. VIKWAZO VIPO KUKUIMARISHA
Vikwazo vipo KUKUIMARISHA na kukufanya wewe kuwa bora zaidi. Mtoto mdogo akiwa anajifunza kutembea kikwazo kikubwa cha kwanza anachokutana nacho ni kuanguka. Kiufupi, kuanguka ni  kikwazo. Lakini kadiri mtoto anavyotembea na kuanguka ndivyo anakuwa anazidi kuimarika zaidi na kutembea vizuri. Kumbe kazi mojawapo ya vikwazo ni KUKUIMARISHA. Jambo kama hili pia huwa tunaliona kwa mtu anayejifunza kuendesha baiskeli. Siku za mwanzo za uendeshaji zinakuwa zimejaa maanguko mengi, ila kadiri maanguko haya yanavyokuwa mengi ndivyo mtu anazidi kuwa mwendeshaji mzuri wa baiskeli. Kumbe usiogope kuanguka Wala kukutana na changamoto. Hizi zipo kukuimarisha wewe na kukuandaa kwa ajili ya maisha bora ya baadaye.

2. VIKWAZO VINAKUPIMA KAMA KWELI UNAKIHITAJI HICHO KITU AU LA!
Katika hii dunia kuna watu wa aina tatu. Aina ya kwanza ni wale ambao wanatamani kupata mambo mazuri ila wapo wamelala, aina ya pili ni wale wanaopenda kupata vitu vizuri na wanaishia kuongea ongea tu kwa . Mwisho ni wale wanaopenda mazuri na wanachukua hatua ili kufanikisha kile wanachotaka. Ni aina ya tatu ambao huwa wanafanikiwa Sana. Kumbe, vikwazo huwa vinatokea kwanza kuwatofautisha watu na kubaki na watu sahihi.

Vikwazo vipo kuona kweli umejitoa kuhakikisha unafanikisha kile ulichopanga au ndiyo unasema sema tu. Kadiri unavyozidi kuonesha kuwa wewe ni king’anganizi kwelikweli, Basi kinachofuata ni vikwazo kukaa pembeni ili kukupisha wewe upate kile unachotaka.

3. VIKWAZO VINAKUANDAA KUWA MKUBWA
Kuna hadithi kuwa zamani katika baadhi ya jamii kipimo cha kuwa umekua mtu mzima na unastahili kuoa  kilikuwa ni wewe kuhakikisha umemuua mnyama mkali kama simba. Yaani, kwamba ulipaswa kupambana na kikwazo kikubwa na kukishinda na hapo ndipo walikuwa wanasema, ooh kweli huyu ndugu yetu amekua. Hata katika maisha ya kawaida haijalishi wewe mkubwa kiasi gani unapokutana na vikwazo vinakukuza  zaidi ya vile ulivyokuwa mwanzo.

Makala inayohusiana na hii: Kutana Na Watu Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo

https://songambeleblog.blogspot.com/2020/10/matatizo-vikwazo-na-changamoto-humtokea.html

4. VIKWAZO VINAKUJENGA NA KUKUFANYA UWE TAYARI KUKABILIANA NA VIKWAZO VINGINE
Ukiweza kutatua na kupambana na changamoto unapokutana nazo, utakuwa na uwezo wa KUKABILIANA NA changamoto nyingine zitakazotokea maishani mwako. Utakuwa unajua mchakato wa KUKABILIANA na changamoto hata Kama hazitakuwa zilezile

5. CHANGAMOTO ZINAKUFANYA MTU WA WATU
Kuna changamoto ambazo huwezi kuzitatua wewe kama wewe. Unasukumwa kukutana na wengine ambao mtashirikiana kwenye kuzitatua hizo changamoto na hivyo kukufanya wewe kuwa mtu wa watu.

SABABU YA NYONGEZA: VIKWAZO VINAKUFANYA WEWE UYAKUBALI MAFANIKIO YAKO UNAPOYAFIKIA
Pale unapokuwa unalifanyia kazi lengo lako na ukakutana na changamoto nyingi, baadaye unapolifikia Hilo lengo unaheshimu mafanikio yako.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X