TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-97 tatizo ni uvivu


Ewe mvivu mwendee chungu, uzitazame njia zake ili upate kujifunza kwake.

Haya ni meneno yaliyoandikwa katika Biblia takatifu  yakikutaka wewe kwenda kwa viumbe vidogo kabisa hapa duniani ili upate kujifunza.

1. Viumbe hawa ni wadogo ila wana Fanya kazi kwa mpangilio na kwa akili ya hali ya juu sana. Kumbe udogo wako (uwe wa kiumbo au kiumri) haupaswi kuwa chanzo cha uvivu. Badala yake unapaswa kuwa chanzo cha uchapakazi. Hauhitaji kuwa mkubwa ili ufanye kazi fulani. Hauhutaji elimu kubwa sana, ili uanze. Kile unachohitaji ni kile ambacho unacho sasa hivi.

Ebu sikia maneno aliyoambiwa Musa alipokuwa akikataa kwenda kuwaokoa waisrael kutoka misri! Una nini mkoni mwako?

Sasa na wewe una nini mkononi mwako? Anzia hapo ulipo tumia kile ulichonacho utajikuta unapata kile ambacho haukuwa nacho.

Sasa bila shaka unajiuliza Nina nini?
Una vitu vitatu vikuu ka ambavyo nimevieleza kwenye Kitabu changu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA(volume-1)
Navyo ni
>>>akili
>>>nguvu
>>>muda

Kama utavutumia vizuri vitu hivi basi utafikia hatua kubwa sana.
ACHA UVIVU, WEKA KAZI

2. VIUMBE HAWA HAWANA AKIDA wala kiongozi.
Tumezoea kila mara kwamba bila uongozi vitu haviendi vizuri. Lakini viumbe hawa wana mtazamo wa tofauti. Bila ya uongozi, bila ya kusukumwa wanafanya kazi kwa bidii kubwa sana.

Kwa kipindi kirefu sana nimekuwa nikifuatilia tabia za watu, nimegudua watu walio wengi bila ya uongozi kazi haifanyiki. Akiwepo kiongozi kazi wanafanya kwa bidii, akiondoka anaondoka na juhudi za watu! Je, wewe ni mmoja wapo? Ebu sikia maneno haya. Acha uvivu badala yake mwendee Chungu ili upate kujifunza kwake.

Sasa hawa Chungu ndio akina nani?
Kamusi ya kiswahili sanifu inawazungumzia Chungu kama ifuatavyo; viumbe wadogo, mchwa

Je, katika hali ya kawaida tunao viumbe hawa kwenye mazingira yetu?
Jibu ni ndio na hapana.
Kama wewe unaweza kuchapa kazi kwa bidii bila kusukumwa na mtu basi wewe una sifa za Chungu.

Kama wewe ni mzembe unasubiri kusukumwa, ili ufanye kazi basi wewe sifa hizi hauna.

ACHA UTANI, KUWA MCHWA MWaKA 2017
IGA KWA MCHWA!

Sasa unaweza kupata vitabu viwili ambavyo nimeandika mimi kwa mkono Wangu kwa shilingi 14,000/- tu! Badaya ya sh. ~20,000~

Tuma pesa kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA

kama unahitaji kitabu kimoja wapo, bei yale hii hapa,
KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI-soft copy tsh. 8000/-

TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA (volume-1) sh. 6000/-
Vitabu vyote ni soft copy, karibuni sana.

ulikuwa nami
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X