Sheria Muhimu Ambayo Unahitaji Kuiehshimu.


habari za leo rafiki na dugu msomaji wa makala za songa mbele blog karibuni sana katika makala za siku ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya kitakachobadilisha mwelekeo wa maisha yetu ya kila siku na kuhakikisha kwamba tunasonga mbele.
tupo katika dunia ambayo imejaa sheria za kila aina. zipo sheria za serikali kuu, sheria za serikali zetu za mitaa, sheria ambazo huwa zinatuongoza sisi katika vikundi vyetu mbali. pengine wewe ni mwanafunzi upo shuleni kuna sheria hapo shuleni, au labda wewe ni mwajiliwa basi kuna shera za hapo kazini.
siku zote ukizifuata sheria hizi lazima utaishi maisha yenye furaha sana. na utafurahia uwepo wako hapa duniani. leo hii naendad kukushirikisha sheria moja ya muhimu sana, ambayo huhitaji mtu wa kukushurutisha ili uifuate lakini ni shera muhimu ambayo kama utaifuata itaongeza matokeo yako ya sasa na kuyafanya yawe zaidi kwa kadri utakavyo taka wewe mwenyewe.
 sheria yenyewe inaitwa sheria  ya kuzidisha. sheria hii ya kuzidisha ni sheria ambayo imekuwepo tangu zamani sana za mababu zetu mpaka leo ambapo unasoma makala hii. Sharia hii ya kuzidisha imejengwa juu ya msingi wa kwamba ili uweze kupata kile unachohitaji lazima uwe  tayari kuwekeza kitu kidogo kwa sasa ili uweze kupata kitu kikubwa sana hapo. Hii huwa inaonekana hata katika hali ya kawaida ya maisha ya kila siku. Chukulia mfano wa mkulima ambaye analima kwenye shamba lake anahitaji kupanda. Anapanda mbegu ili hali akijua kwamba mbegu zake zitaongezeka na kuwa nyingi sana.
Lakini kumbuka kwamba mkulima huyu angeweza kuchukua mbegu hizi na kuzipeleka kuziuza sokoni ili aweze kupata pesa. Lakini kutokana na kanuni hii ya kuzidisha aananpanda mbegu ili hali akijua kwamba anatapata zaidi ya kile alichopanda. Kumbe sheria hii ya  kuzidisha ni muhimu sana, kuifahamu. Hii itakusaidia sana kujiua kwamba ili uweze kutoka tu hapo ulipo na kuweza kufika unapotaka kufika tena kwa kishindo unahitaji kuwa tayari kupanda kitu kidogo ambacho ndicho kitakachokutoa hapo ulipo na kuhakikisha kwamba unafika kileleni.
Mambo y akufanya siku ya leo.
1.     Tafuta mambo  matano  ambayo utaenda kuyafanya, kwa kutumia kanuni hii ya kuzidisha.
2.     Yaandike chini na angalia ni jambo gni ambalo unaenda kuanza nalo na lipi litafuata kwa kufanywa.
3.     Yape ukomo w a kukamilika. Maana kila kitu huwa kina muda wake wa kukamilika. Anza leo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X