Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa najiuliza swali “ kwa nini mambo mapya yanazidi kugundulika kila siku?
Sikuwahi kupata jibu zuri la mambo haya mpaka pale nikipomaliza kidato cha sita, ndipo nilipokuja kugundua jambo hili. Swali jingine nililokuwa nikijiuliza ni “ je, kuna uwezekano wa kugundua mambo mapya kila siku”.
Ni mara myingi sana mimi na rafiki zangu tumeulizana maswali mengi sana kuhusu mambo tunapendelea na kazi tunazozipenda. Kila mtu amekuwa na mtazamo wake huku kukiwa na baadhi ya marafiki zangu ambao huniambia wao wangependa kuigiza, wengine kuimba na wengine kucheza mpira.
Je, wewe unapendelea nini?
Je, unajua unaweza kutengeneza pesa kutoka kwenye kile unachokipendelea?
Ni ukweli kwamba kadri unavyopita kwenye maisha unajikuta kuna mambo unafanya vizuri zaidi. Kumbe kila mtu ana zawadi na kipaji ambavyo kazaliwa navyo na ambavyo havifanani na vya mtu mwingine.
Hapa ndipo tunakuja kujua kwa nini watu huwa hawaishi kugundua mambo mapya. Kwa sababu hivi vipaji na zawadi amabvyo kila mtu anavyo hutofautiana kati ya mtu na mtu.
Vipaji hivi vipo tu kwenye akili yako na hugunduliwa kadri mtu unavyokua.
Ni mara nyingi sana nimesikia rafiki zangu wakisema “ mimi ni mwigizaji ila nasubiri kwanza nipate kazi “
mwingine atakuambia “Mimi ni mwimbaji ila hicho ni kitu ninachokipenda tu”
Na mwingine atasema “Mimi ni mchekeshaji ila siwezi kutengeneza pesa kupitia hilo”
Kuna msemo mmoja wa kiingereza unaosema “DIG GOLD WHERE YOU ARE” ukimaanisha ” chimba dhahabu popote pale ulipo”.
Kumbe kipaji chako chochote kile ulichonacho ndicho unaweza kukitumia kutengeneza pesa. Kwa sababu kipaji chako ni cha kipekee na ndicho kitakachopelekea wewe kugundua jambo jipya kwenye dunia hii.
Kitu cha msingi hapa ni kwamba lazima uwe na kusudi.
Na kusudi litokane na kipaji chako. Hili ndilo litakaloonesha sababu za wewe kuishi. Kusudi ni kama mfumo wa ndani ambao utakuongoza wewe ufanye nini.
Kipaji hiki ni cha kipekee na kimo ndani yako. Kutokana na kile wewe unapenda na unakifanya hata huwezi kuona kama unatumia mda mwingi.
Unaweza kuamka asubuhi na mapema bila hata wewe kujiuliza kwa nini unafanya hivyo.
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasusha kutoka kwenye blogu hii
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante