Hili ni Kosa Amabalo Watumiaji Wengi wa Mtandao Hufanya


Habari za leo msomaji wa SONGA MBELE BLOG
Ni imani yangu unaendelea vyema kupiga hatua na kuweza kufikia mafanikio. Hongera sana kwa siku njema ya leo na karibu sana katika somo la leo.

Ni ukweli kwamba watu wengi hupenda kushinda katika mitandao ya kijamii wakichati na kubadilishana mawazo na marafiki zao. Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu ambao hushinda mitandaoni hawanufaiki nayo hata kidogo. Ni wazi kwamba wanapata nafasi nzuri ya kuchati  na watu wengi, lakini asilimia tisini na tisa (99%) ya watu anichati nao hawajui wanaweza kupata nini kwake.
Je wewe ni mmoja wapo? Je, watu unaochati nao wanajua wanaweza kupata nini kwako? Hujachelewa. Kusoma kwako hapa ndio mkombozi wako.

Soma zaidi; Unahitaji Kufanya Haya Kila Siku

Sasa ujue ukweli kuhusu mitandao ya kijamii.
Mitandao ya kijamii ni vijiwe ambapo watu hukutana kupiga soga. Hii ni kawaida kwa wengi kukutana vijiweni,  mitaani kwetu ili kubadilishana mawazo. Kwa kawaida mtu akitoka kwenye kijiwe cha mtaani huwa anaeleka nyumbani kwake.
Je wewe ukitoka kwwnye kijiwe cha facebook nyumbani kwako ni wapi? Nyumbani kwako ni kwenye blogu yako. Kwa kawaida mtu akienda kijiweni anaweza kuwakaribisha watu aliokutana nao kijiweni kwake nyumbani kwake. Je wewe ukitoka kwenye mutandao ya kijamii kuna watu unawakaribisha nyumbani kwako?
Blogu yako ni nyumbani kwako na hakikisha unawakarbisha marafiki zako nyumbanibkwako anbapo ni kwenye blogu yako. Ukishawakaribisha  hapo ndipo unakuwa na uwezo wa kuwaambia ni bidhaa gani inapatikana kwako na jinsi gani wanaweza kuipata.
Kwa namna hiyo utakuwa umepata nafasi nzuri ya kuitumia mitandao ya kijamii.

Soma zaidi; Yafahamu Mambo Ambayo Huwezi Kujifunza Shuleni

Nitafanyaje sasa?
Jambo la msingi sana kwa siku ya leo ninkwamba unatakiwa ufungue blogu yako.  Ambapo utakuwa unawaalika watu wanaotoka vijiweni kuja nyumbani kwako.

Kwa nini blogu?
Zama zimebadilika, maisha yamebadilika na wewe badilika.
Tupo kwenye zama za taarifa ambapo mtu mwenye tarifa sahihi na anaitoa kwa wakati sahihi na ndiye mwenye uwezo wa kutengeneza pesa.
Zama za taarifa zinamhitaji kila mtu awe na blogu yake ili apate nafasi ya kutangaza biashara yake kwa watu wengi ndani ya muda kidogo. Katika dunia ya sasa unaweza kuwa maarufu ndani ya dakika 15! Usiikose fursa hii adimu
Wakati ni sasa, badilika sasa chukua hatua na anza sasa.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


2 responses to “Hili ni Kosa Amabalo Watumiaji Wengi wa Mtandao Hufanya”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X