Ifahamu Tofauti Kati Yako na Huyu.


Matokeo yako ya sasa hayana cha kufanya na maisha yako ya baadae.
Hivi kama wewe kwa sasa ni maskini ni kweli kwamba wewe utaendelea kuwa maskini?
Hivi kama wewe unaingiza elfu kumi kwa siku ni kweli kwamba utaendelea kuwa unaingiza elfu kumi.

Soma;Ijue Siri YaBabiloni kuwa mji tajiri kuliko yote duniani

Hapa jibu la haraka ni hapana. Kwa kawaida huwa tunacheza mchezo wa kuijilinganisha na watu wengine. Na pale tunapojilinganisha na watu ambao wametuzidi kimafanikio basi huwa tunajiona wanyonge na na watu wa hali ya chini sana.

Mtazamo kwamba wewe unaofautiana na mtu yeyote anyetembea katika sayari ya tatu ni ujinga. Wewe ni sawa na mtu yeyote aliye katika sayari hii na wote ni sawa na wewe.kwa hiyo sote tuna uwezo sawa, tofauti hutokea akilini mwako.

Hii mara nyingi huonekana kwa watoto wadogo, wakiambiwa kwamba wao ni wajinga basi na wao huchukulia hivyohivyo kwa kufuata kile ambacho wanambiwa. Lakini pia wakiambiwa wana akili na uwezo mkubwa ,basi huweza kufanya hivyo na kufikia matokeo makubwa

Kuna vitu unaamini ambavyo uliingizwa tangu utotoni, na ukiamini hivyo hivyo basi vitakuja kukuathiri katika utendaji wako. Ni muhimu sana kubadili mtazamo wako.

Kwa hiyo tofauti kubwa sana kati ya wewe na watu wengine ni mtazamo.  Badili mtazamo wako iki uweze kukua zaidi na kuendelea mbele ili kufikia malengo yako.

Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X