Ijue Siku Rafiki Kwako


Leo ni siku nzuri
Leo ndio rafiki yako
Leo ishakuwa
Leo ndo muda pekee ulionao

Kama leo ndo ingekuwa siku pekee ya kuishi duniani ungeitumiaje?

Leo ni muhimu
Mara nyingi tunaisahau leo. Hatuishi leo. Hatuthamini muda tulionao leo, na kufikiri tunasubiri mpaka kesho.
Hata hivyo kesho huwa haifiki.
Kesho hutupa matumaini.
Lakini leo yako inaonekana katika kile tunachokifanya.

Leo ndo rafiki yako
Kesho inaweza kukupa vitu vipya, kuponya majeraha ya jana na kukupa matumaini ya baadae.
Ikumbukwe kila kitu hufanyika leo. Leo ndio muda muafaka wa kukuza mawazo yetu na kuyaweka katika matendo.

Kesho ni siku ambayo iko mbali usiitegemee kesho ije ikuokoe.
Leo ni siku ambayo unayo

  • Ishi tabia zako: upo jinsi ulivyo kwa sababu ya kile unachokifanya. Hili ndilo huonesha tabia zako, haupo jinsi ulivyo kwa sababu ya kile unachotegemea kufanya kesho.
  • Anza: kama una lengo la kupiga hatua anza leo: achana na maneno kama vile ntasoma kesho, nitafanya mazoezi kesho, nitaanzisha blogu yangu kesho. Mda wa kuanza ni sasa, amua sasa badilika sasa.
  • Maliza:  maliza kila kitu ambacho ulipaswa kukifanya leo. Yaani hakikisha hakuna kitu kimebaki ndani yako ambacho kilipaswa kufanyika leo. Toa kila kitu ndani yako usibanie kile kitu ambacho unafikiri unaweza kufanya. Weka juhudi zako zote kwenye kile ambacho umeamua kufanya. Usiguse kitu chochote kwa juujuu bali kifanye kwa uhakika.
  • Tunza muda. Kesho inaweza kuchelewa sana kwa wewe kupata fursa nyingine, na kuanzisha kitu cha ndoto yako. Kumbe muda ni sasa, amua sasa na badilika sasa.
  • Ndoto ya kesho ifanye leo: Najua wazi kwamba kesho tunazo nyingi zinakuja. Lakini kile tunachofanya leo ni muhimu. Kesho inaweza kutupa ahadi nyingi sana. Lakini leo ndo kila kitu 
Je leo unaenda kufanya nini?

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane 
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante
Unaweza kuupenda ukurasa wangu wa facebook kupitia 
fb.me/songambeleblog


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X