Je Shule na Maisha Vinaendana?


Habari za leo rafiki na msomaji wa SONGA MBELE BLOG
Ni imani yangu unaendelea vyema katika safari ya kuelekea mafanikio ambayo umeipanga.
Leo tunaenda kuona mambo fulani ambayo huwa tunajifunza shuleni lakini katika hali halisi ya maisha huwa ni tofauti.

Kwa kawaida watu wengi sana wana mtazamo kwamba wasome au wasomeshe watoto, katika shule nzuri, wapate maksi nzuri ili wakaajiriwe katika makampuni makubwa. Hayo ndio mambo ambayo huwa tunajifunza shuleni na walimu wetu hutusitiza hivyo. Wazazi wetu pia husisitiza jambo kama hilo
Lakini katika hali halisi ya maisha mambo huwa ni tofauti na tunavyofikria.

je, shule na maisha huenda a

Je, shuleni huwa tunajifunza nini cha zaidi?

1. Uoga wa kufanya makosa na kushindwa.
Hivi mwanafunzi akishindwa mtihani mwalimu huwa anamfanyaje?
Hivi mwanafunzi asipofanya vizuri mzazi huwa anajisikiaje?
Ni kawaida kwamba mwanafunzi akifanya vibaya huwa anaadhibiwa vikali kuonesha kwamba hapaswi kufanya kosa lolote maishani mwake.
Tena nakumbuka adhabu kubwa sana iliyokuwa inayolewa shuleni ni adhabu ya kulima.
Hii bado inajenga picha mbaya nakuonesha kwamba kilimo sio kitu kizuri na kinapaswa kufanywa na waharifu.
Hii ndiyo hali halisi ya shule.

Je, hali ikoje kwenye maisha?
Hali ni tofauti kabisa kwenye hali ya maisha. Kwa sababu katika safari ya mafanikio huwa hakuna njia nyoofu ambayo haina vikwazo.
Safari ya mafanikio imejaa vikwazo vingi ambavyo tunapaswa kuvitatua ili kuweza kufikia mafanikio. Kadri tunavyotatua vikwazo ndivyo tunavyozidi kusongambele kuelekea mafanikio. Hakuna mtu ambaye amefikia mafanikio bila kupata changamoto na vikwazo vingi. Ndio maana watu waliofikia mafanikio makubwa hawakumaliza shule.
Watu kama Thomas Edison mwanzilishi wa kampuni ya umeme ambyo ilitengeneza taa za umeme tunzaotumia leo.
Mark Zuberbeck mwanzilishi wa mtandao wa facebook, Bill Gates mwanzilishi wa kampuni ya microsoft

soma zaidi hapa; Kama Hawa Waliweza Kwa Nini Wewe Usiweze

2. Uoga wa kukosa kazi.
Hali halisi ya shule siku zote huwa ni kwamba usome kwenye shule nzuri, upate elimu nzuri, ukaajiriwe kwenye kampuni au shirika zuri au serikalini  na upate mshahara mzuri.
Hii huwa inajenga hofu kwamba usiopata maksi nzuri basi wewe umeshindwa maisha. Kutokana na kuogopa huku wanafunzi huwa wanajikuta wanafanya kitu ambacho hawakipendi. Hii inatokana kwamba wanasoma kwa lazima wakilazimika kupata maksi nzuri ili wasije wakakosa ajira. Lakini kiuhalisia sio kwamba wanapenda kusoma. Mitihani ikiondolewa basi huwezi kumwona mwanafunzi anajihangaisha kusoma. Hapa ni kwamba mwanafunzi anafanya kitu asichokipenda.
Ndio maana wanafunzi wanaofaulu na maksi nzuri shuleni huwa hawafanyi vizuri katika maisha. Mtu aliyepata A katika masomo maana yake hajafanya kosa , na maisha yake yote hatapenda kukosea hata kitu kimoja. Hali ya kukosea humfanya myonge na kuonekana kama vile hawezi.

Sasa nifanyeje?
Kabla sijaendelea zaidi ningependa kukuuliza swali moja la msigi sana.
Je umewahi kumwona mtu ambaye hapendi shule lakini anapenda kusoma vitabu vya maarifa?
Je unajua ni kwa nini?
Hii ni kwa sababu katika vitabu vya maarifa kuna elimu ambayo hutolewa ambayo haikughalimu na haikuhitaji uifanyie mtihani ili utafute maksi nzuri na kufaulu.

Soma zaidi hapa;Faida sita (06) za Kusoma Vitabu na Makala za Kuelimisha

Soma zaidi hapa; Kumbe Huwa Hawafanyi Haya

Usiogope kushindwa. Mwandishi mmoja wa vitabu katika karne hii ya ishirini na moja Robert Kiyosaki ansema kwamba “watu wengi ambao hawajafikia mafanikio ni kwa sababu wameshindwa kushindwa mara nyingi”  usiogope kushindwa chukua hatua na songambele, na kufikia mafanikio ya malengo yako.

Soma zaidi hapa: Mambo Manne (04) Ambayo Huwezi kujifunza Shuleni

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X