Je, Unaijua Kauli Haribifu Kwenye Maisha Yako?


Hii ni kauli moja ambayo watu wengi sana hupenda kuitumia.  Kauli hii watu wengi sana hupenda kuitumia sana hasa pale mtu anapoogopa atafanya jambo na atashindwa. Kauli hii ni mbaya sana maana husababisha watu kurudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Je kauli hii ni ipi?
Kauli ye hewe ni hii hapa  “itakuwaje”?
Watu wengi sana hupenda kusema

  •  itakuwaje kama nitashindwa
  • Itakuwaje kama sitafika
  • Itakuwaje biashara zangu zisipofanikiwa
Kwa bahati mbaya watu ambao hutumia kauli hii huwa hawajishughulishi na kufikria ni kwa namna gani wanaweza kuelekea mbele na kufanikiwa zaidi, badala yake huishia tu kusema itakuwaje.


Kumbe yatupasa kuchukua hatua bila kujiwekea vikwazo. Kila kitu kinaweza kuwa jinsi kilivyo kwa sababu ya jinsi wewe tunavyofikria. Ukiogopa kufanya jambo fulani kwa sababu utashindwa, basi maisha yako unaweza kuwa mtu wa kutochukua hatua. Usikubali hilo likutokee wewe.

Binadamu alivyo ni mtu wa kuchukua hatua na kupambana sio mtu wa kuogopa, akijiuliza itakuwaje.

Mtoto akizaliwa,  baada ya mda anaanza kutambaa, hivi kama mtoto angejisemea  “itakuwaje pale nitakapotambaa na kugusa moto” unadhani angetambaa? Nina uhakika uhakika mtoto angeamua kutotambaa kwa sababu mambo hasi ambayo yanaweza kujitokeza baada mtoto kutambaa ni mengi sana.
Au kama mtoto angejiuliza  “itakuaaje pale nitakapoanza kutembea na kuanguka?” Basi bila shaka mtoto angeamua kutotembea kwa sababu ya kuogopa kuanguka.

Ni wazi kabisa binadamu akizaliwa huwa ni mtu wa kuchukua hatua bila kujali ni kitu gani kitakuja kutokea mbeleni.

Swali # je ni kitu gani ambacho husababisha ubunifu huu kupotea?
Ubunifu huu na kuchukua hatua ambayo ni asili ya binadamu hupotea baada ya mtoto kuanza kukua, ambapo watoto huingiziwa mawazo hasi. Suala hili hupelekea mtoto kuacha kuchukua hatua. Hapa ndipo watoto huanza kuingizwa katika ile hali ya itakuwaje, na kupoteza ubunifu wake na nia yake ya kuchukua hatua ili aweze kufikia mafanikio.

Naamini hakuna mzazi au mlezi ambaye angefurahia mtoto wake kutotembea. Hii inaonesha kwamba hakuna mzazi ambaye hapendi mafanikio kwa mtoto wake. Kupenda mafanikio ni haki ya kila mtu. Sasa kwa nini unajiwekea vikwazo ili usiweze kuendelea mbele?
Amua sasa, badilika sasa, chukua hatua na songa mbele.
Usijali maneno ya kukatisha tamaa, kuwa kama mtoto mdogo na kuwa na shauku ya kujua kila kitu na kufanya kila kitu bila kujiwekea vikwazo

Endelea kusoma makala  za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante

Unaweza kuupenda ukurasa wangu wa facebook kupitia fb.me/songambeleblog


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X