Habari za leo ndugu msomaji wa songambeleblog.blogspot.com Ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuimarisha maisha yako na kufikia mafanikio.
Leo tunaenda kuangalia jambo muhimu sana katika maisha yako ambalo linaweza kuwa limekutokea au unaweza kukutana nalo ktika safari ya kutafuta mafanikio
Jambo lenyewe ni kukata tamaa. Hili huweza kutokea baada ya kujaribu jambo flani na kushindwa kufikia hatua flani uliyokuwa unaitaka au uliyokuwa unatarajia kufikia.Unaweza kuwa umelifanya mara moja au umerudia mara nyingi lakini bado hujafanikiwa.Lakini pia yaweza kuwa ni ndugu au jamaa zako wa karibu,ambao wanajaribu kukwambia usiendelee mbele huku wakitaja changamoto na maneno kadha wa kadha za kukatisha tamaa.
Habari njema ni kwamba usikate tamaa bado unaweza kulifanya jambo ambalo unafikria na kufanikiwa,tena vizuri sana.
Ebu tuone baadhi ya watu ambao wameweza kupambanana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana japo wamepitia vikwazo vya aina mbalimbali.
Mark Zuckerberg huyu ni mwanzilishi wa mtandao maarufu sana duniani,mtandao wa facebook.Alipoanzisha facebook watu wengi walimcheka sana,wakidhani haiwezekani kwa yeye kufanikiwa.Tena alipofukuzwa chuo ndipo walisema ngoja tuone ndoto zake zitaishia wapi? Lakini kutokana kwamba yeye alikuwa na ndoto kubwa sana ndani yake ambayo aliiona itakuja kukua,aliifanyia kazi. Mpaka sasa facebook ndo mtandao mkubwa sana wenye watu wengi zaidi duniani. Watu waliokuwa wanamcheka ndio watu wenye akaunti facebook.
Fundisho Beba ndoto yako wewe ndo mwenye maono na wewe ndio unayeona uendako.Hao wengine wanaokukatisha tamaa hawawezi kuona kile ambacho wewe unakiona.Wewe ndo mtu pekee mwenye uwezo wa kuona mbali sana,hakikisha kile ambacho unakiona wewe unakiendea nakukifikia.Usifumbe macho wala kurudi nyuma endelea mbele wala usipite pembeni.
Henry Ford.Huyu ni mwanzilishi wa magari maarufu sana duniani ya V-8.Lakini siri iliyo nyuma ya mafanikio ndiyo nataka kuongelea kwa ufupi sana.
Ford aliwaambia wahandisi wake watengeneze ramani ya ingini ya silinda nane.walipoiwasilisha ramani akawaambia anzeni kuitengeneza.
Wakamwambia “haiwezekani”
kawambia “anzeni”
Ilibidi waanze kwa sababu hawakutaka kupoteza kazi.Miezi sita ilipita na miezi sita mingine ikafuata.Mwaka mmoja baadae Ford alikuja kuwaangalia wahandisi wake,lakini bado walimwambia haiwezekani akwambia “endelea kwani naihitaji”
Baadae wakaitrngeza na ndio mwanzo wa kutengeneza magari maarufu sana ya V-8.
Fundisho Usijiwekee vikwazo mwenyewe kabla ya kuanza kazi.Anza kufanya kazi na changamoto zitakazojitokeza zirekebishe.Changamoto lazima zitokee na uwe tayari kukabikiana nazo.
Thomas Edison huyu ndiye aliyegundua taa za umeme bila shaka bila ya huyu umeme unaowaka usingekuwepo.Alifanya makosa zaidi ya mara elfu kumi lakini hakukata tamaa.Alipoulizwa kwa nini ulifanya makosa zaidi ya mara elfu kumi alisema ” nilikuwa naangalia kitu gani sikufanya katika hizo mara elfu kumi.
Fundisho Usione haya kurekebisha kile ulichokosea,kwa kufanya hivi utaweza kufikia mafanikio ya juu sana.
Basi ndugu msomaji hii ni ishara tosha kwamba hata wewe hiyo ndoto yako uliyonayo inaweza kufanikiwa ,tena vizuri sana.
Kama hawa waliweza kupitia changamoto nyingi na kufanikiwa.kwa nini usifanikiwe anza sasa na utafanikiwa.Anza sasa maana hakuna mda mwingine kama sasa na siku nyingine kama leo.siku tunayoianza kesho ni ya tofauti kabisa na leo.kwa hiyo nasisitiza tena anza sasa.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391
Ni mimi
Ndugu yako,Godius Rweyongeza
Tuwasiliane godiusrweyongeza1@gmail.com
0756848391
Asante
Endelea kufuatilia makala za kuelimisha na kuhamasisha kuyoka kwenye blogu hij.
One response to “Kama Hawa Wameweza Kwa Nini Wewe Usiweze;Usikate Tamaa Songa Mbele.”
Kazi nzuri ndg songambele