Kwa Nini Kuzaliwa Maskini sio Dhambi Lakini Kufa Maskini ni Dhambi


“Kuzaliwa maskini sio dhambi lakini kufa maskini ni dhambi” hii ni kauli maarufu iliyotolewa na blionea Bill Gates.
Tunapozaliwa hakuna ambaye huwa anachagua azaliwe wapi na azaliwe na nan. Ni bahati tu kwamba kila mmoja huwa anajikuta kazaliwa katika mazingira ambayo yumo. Haijalishi ni katika mazingira ya kitajiri au kimasikini bado kote ni bahati tu.

Jambo la msingi sio kuzungumzia umezaliwa wapi ila ni kuona thamani yako na uwepo wako hapa duniani. Tunapozaliwa Tunapewa zawadi za msingi sana ambazo kama kila mtu atazitumia vizuri, zitamletea mafanikio makubwa sana.
Zawadi hizo ni hizi hapa:

1. Mda.
Je unautumiaje mda wako?
Je unauuza mda wako kwa wayu qbb wako kwa watuKila binadamu amepewa mda wa saa 24 kwa siku. Hakuna aliyepewa zaidi, au pungufu. Kama wewe utautumia vzuri mda wako utajijengea faida kubwa sana. Unaweza kuamua kuuza mda wako au kuutumia mwenyewe mda wako na hata kununua mda wa mtu mwingine.
Matajirwa dunia hii ni wale wanaoutumia vizuri mda wao.

2. Nguvu
Kila mmoja wetu amepewa nguvu za kutumia, hata kama upo kwenye hali gani lakini bado unazo nguvu na uwezo wa kufanya mambo makubwa ya kukuletea maendeleo.

3.Akili
Hii ni zawadi nyingine nzuri sana ambayo umepewa. Kila mwanadamu amepewa akili ambazo kama atazitumia vizuri, zitamsaidia kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo. Akili inafanya maamuzi mengi sana, kama itaamua kwamba nataka nifanikiwe utafanikiwa, kama itasema sitaki mafanikio basi hautapata. Itumie akili yako kufikiri.
Tajiri ni yule anyefikiri kwenda kulia na maskini ni yule anyefikiri kwenda kushoto. Fikiri ni kwa jinsi gani unaweza kutoa huduma kwa jamii yako. Ukiwa na jambo ambalo unafikiri linaweza kusaidia watu, kama utawasaidia utafaidila sana.

Huu ndio  ukweli ulio nyuma ya “kuzaliwa maskini sio dhambi lakini kufa maskini ni dhambi”.
Kumbe wakati wa kubadilisha hali yako ni sasa na hakuna mda mwingine kama sasa, anza sasa na badilika sasa.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane 0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.

Endeles kutembelea blogu hii kwa makala za kuelimisha ma kuhamasisha. Zaid


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X