Mambo Ya Kufanya Kabla na Baada ya Semina


Kwa kawaida katika semina huwa tunapata nafasi ya kuungana na kukutana na watu wengi sana. Watu waliotoka maeneo mbalimbali na kila mtu akiwa na shughuli zake anazofanya. Utakutana na watu waliovaa vuzuri na kupendeza na wengine wakiwa wamevaa kawaida. Je, wewe utaongea na akina nani? Je, utawaambia nini hawa?

Hapa ndipo walipo marafiki zako wapya ambao unaenda kukutana nao. Usijisikie mpweke nakujionakama umepotea njia.
Soma; Tabia tano zitakazokufanya uwe na furaha

mambo ya kuzingatia kabla na baada ya semina
Kabla hujaenda kwenye tukio.
Ongelea kuhusu tukio na unaweza kuwapa taarifa marafiki zako kwamba wewe utakuwepo. Fuatilia kujua ni akina nani watakuwepo? Nani atatoa semina? Weka picha yako ambayo umepiga karibuni ili iwe rahisi kwa watu kukutambua siku ya tukio.
Hakikisha umeandaa kadi za biashara ( business card) za kutosha ili uweze kubadilishana na watu wengine siku ya tukio. 
Soma; Hiki ndio kitu ambacho unacho peke yako
Kuwa wewe kama wewe.
Unapokuwa kwenye semina yawezekana  hujaenda pale kuwakilisha kampuni au shirika lakini upo pale kama wewe. Watu waliopo pale watapenda kujua wewe ni nani?, na wanaweza kupata nini kutoka kwako. Huu ndio muda muafaka wa wewe kujitangaza na kuitangaza biashara yako.
Wakati wa semina
Wakati wa semina kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia. Kama kuna watu wengi sana ni muhimu kufahamu kwamba nyote mko pale kwa lengo moja ambalo linawakutanisha. Kutana na watu wengi, tafuta marafiki wengi, wateja wengi,  na watu wa kushirikiana nao katika biashara.
  • Fika mapema kwenye eneo la tukio unaweza kufika nusu saa kabla. Hii itakupa mwanya wa kuonana na watu wengi zaidi.
  • Jitambulishe mwenyewe unapokutana na watu wapya na ongeza jina la kampuni yako au biashara yako. Mfano unaweza kusema “habari mimi naitwa Godius Rweyongeza ni mwazilishi na mwendeshaji wa mtandao wa SONGA MBELE
  • Usitumie muda mwingi kuongea na mtu mmoja au kikundi kimoja cha watu. Tumia kati ya dakika tano mpaka saba kuongea na mtu au kikundi kimoja.
Soma;Kupe hawa wananyonya muda wako kila siku
  • Mwisho wa mazungumuzo yenu badilishaneni kadi za biashara ( business card). Usisahau kuchukua za kwao.
  • Kama hukumbuki jina la mtu mwishoni mwa mazungumuzo ni vizuri kumuuliza.
Baada ya tukio
Ukifika nyumbani chukua kadi za biashara ambazo ulizikusanya wakati wa semina na wakumbushe watu kuhusu jambo mliloongelea wakati wa semina. Hii itasababisha kupanua biashara yako zaifi na zaidi na kukuza mahusiano mazuri.
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X