Maneno ya Kuepuka Kuongea Kila Siku.


Unapohitaji kupata kitu ambacho hakimo kwenye bajeti usiseme “siwezi kupata hicho”
Watoto wako wanpohitaji kwenda kucheza na kujumuika na wenzao usiwaambie “sina uwezo”
Mke wako anapotaka vazi zuri usimwambie “ hatuna uwezo.”

Usiwe na mtazamo huu wa uhaba

Badala yake ukihitaji kitu kizuri jisemee  “ nitakipata “
Hata kama hauna pesa karibu ya kununua kile unachohitaji. Angalia kwanza ni vitu gani unahitaji na weka njia ya kukuwezesha kupata pesa ya kuvinunua vitu hivyo.

Usiruhusu kushindwa katika mawazo yako.  Badala yake jenga mtazamo wa ushindi katika kila kitu. Weka  mtazamo wa kipesa wa kukusaidia kufanya kazi. Leo hii kama uko kwenye njia na huoni mwanya wa mafanikio basi badili mwelekeo wako.

Je, wewe dunia unaionaje?
Je, bado unafanya kile kitu ambacho kila mtu alikuwa anafanya na kuleta mafanikio yaleyale.
Kama ni hivyo badili mtazamo wako. Yaone mambo yote katika uchanya. Usitafute kila sababu za kuhakikisha  unakwama.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X