Watu wengi sana wamekuwa wanafikiri safari ya mafanikio ni rahisi sana, na hivyo huingia katika biashara kwa kuwa na mtazamo wa kupata mafanikio tu. Pale inapotokea vikwazo vya aina mbalimbali njiani ndipo mtu huona ugumu wa kazi na kuamua kuacha.
Safari ya mafanikio sio rahisi wala sio safari ya kubashiri, au kubahatisha. Unapoamua kuanza safari ya mafanikio, siku zote lazima utakutana na vikwazo mbalimbali, ambavyo muda mwingine sio rahisi kuvitatua.
Msingi mkubwa sana wa kutatua matatizo yaliyo katika safari ya mafanikio hutegemea imani.
Maisha yetu kimsingi yamejengwa juu ya imani. Imani ambayo ndiyo hutuletea fikra na fikra hutusaidia kutenda. Tunaweza kutumia imani yako kupima matokeo yako. Kumbe imani ni kipimo cha mafanikio. Mfano wapo baadhi ya watu ambao huwa wanaamini kwamba wao siku zote wana mkosi, hawana bahati, na hawataweza kufanikiwa maishani. Kwa kuwa washajiaminisha hivyo ni kweli hawa watu hawawezi kufanikiwa kwa sababu ya imani yao waliyonayo. Pia wapo watu ambao wao hufikiri wanaonewa, wanafanyiwa ubaya na kusumbuliwa. Watu wa aina hii hata kama utafanya jambo jema sana hawataliona kwa sababu wao wanaona wanaonewa na kusumbuliwa. Hayo yote ni matokeo ya imani.
Imani ndio hupelekea kufanywa kwa kile ambacho kinapaswa kufanya na inaiongoza akili, kutoa mawazo kutokea kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa auto suggestion. Auto suggestion ni sehemu ya ubongo ambayo huzalisha mawazo kulingana na imani yako.
Kama unaamini kwamba hata kama utakutana na vikwazo kiasi gani bado utaendelea kupambana mpaka kufikia mafanikio, basi tu utafanikiwa. Huo ndio msingi mkubwa wa imani.
Swali. Je, nisipofanikiwa nimlaumu nani?
Kwa kuwa nilitangulia kusema kuwa tupo tulivyo kwa sababu ya imani zetu. Imani zetu ndizo hutuletea fikra, na fikra zetu ndizo huingia katika matendo. Hivyo pale unaposhindwa kufanikiwa katika maisha jua mtu wa kumlaumu sana ni wewe. Ujilaumu mwenyewe kwa sababu umekuwa ulivyo kwa sababu ya imani yako.
Ni hayo tu kwa leo. Nakutakia safari njema sana ya kuelekea mafanikio.
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii
fb.me/songambeleblog