Sote tunahitaji kuwa na maisha bora na furaha kwenye maisha yetu. Lakini huwa tunakutana na vikwazo na matukio ambayo hutufanya tusiwe na furaha.
Mambo hayo yanaweza kuwa kushughulika na watu wabaya, kufanya kazi maeneo tusiyoyataka na mipango kutokamilika. Hayo na mengine mengi huweza kutuondolea furaha, kuridhika na kuharibu mtazamo wa akili zetu
Kuna uzoefu mbaya wa akili kuweza kutegemea matatizo na kutoridhika pamoja na kuondoa hali ya furaha.
Hii husababisha mtazamo hasi wa akili kiasi kwamba pale tunapokuwa na furaha mtu hutegemea kitu kibaya kutokea na hivyo kuondoa furaha yake.
Ili kuwa mtu mwenye mafanikio lazima kuondoa huu mtazamo hasi na wenye kuharibu.
Mara tunahusisha furaha na mambo ya nje kama vile kutafuta upendo na kwenye starehe.
Hivi vitu vinaweza kuleta furaha lakini usivitegemee. Haupaswi kusubiri matukio mazuri yatokee ili uwe na furaha. Unaweza kujihusisha na maksudi katika vitendo ambavyo huleta furaha.
Je, mabadiliko ya mazingira huweza kutengeneza furaha?
Ingawa furaha huonekana kutokea kwenye matendo ya nje ambapo kwa mda wewe huweza kusahau matatizo na magumu yako. Hii hutokea pale unapofanya kitu ambacho wewe unapenda kufanya unapotulia. Hii hutokea pale tunapopata habari njema au kitu kizuri kinapotokea na kuondoa akili yako katika mambo yanayo kusumbua.
Kiukweli furaha hutokea ndani yako na haitegemei watu au matukio. Hii inaanisha kwamba tunaweza kupaya furaha hata kama tunapitia kwenye hali mbaya. Ukiamini tofauti kutaweka akili yako, furaha na unavyojisikia katika mikono ya watu wengine.
Furaha ni hisia ya ndani, hisia ya kuridhika kukamilika na kutulia. Unapokuwa na furaha hujisikii kuwa na dhiki, hauhofii chochote na haufikrii kitu chochote kibaya.
Nina uhakika umewahi kuwa na furaha katika maisha yako tena mara nyingi. Haijalishi umepitia katika hali gani hata katika hali mbaya lakini bado kuna nyakati za furaha. Unapokuwa na furaha unasahau matatizo yako kwa mda na unafurahia amani ya ndani. Ningependa kukupa baadhi ya tabia ambazo zinzaweza kukupa furaha katika maisha yako.
1.Tafuta furaha katika kitu kidogo kilichokuzunguka.
Usisubirie kitu cha kipekee kutokea, ili uwe na furaha. Mambo ya kipekee hayatokei kila siku lakini kuna mambo madogo ambayo unaweza kufurahia na yapo kwa wingi sana. Hapa kuna baadhi ya mifano.
- Kusoma kitabu kizuri.
- Kupata kifungua kinywa kizuri kabla hujaenda kazini.
- Kutumia mda wako na ndugu zako na uwapendao.