Safari ya ya mafanikio sio ya mchezo mchezo, bali safari ambayo hukuitaji uwe makini na ujiandae sawasawa na kujitoa. Kama utaanza safari ya kimafanikio bila kujitoa sawasawa, na kujiandaa pale utakapokutana na vikwazo mbalimbali kama vile kukata tamaa, kukatishwa tamaa, kupingwa, na visingizio utakwama. unahitaji uwe umejipanga kisawasawa.
Unahitaji kuwa umeweka malengo na mipango ya jinsi gani utaanza mpaka kufikia kileleni
Unaambiwa kati ya biashara kumi ambazo huanza kila mwaka, tisa hufa ndani ya mwaka mmoja, na kati ya zile zinazoendelea moja kati ya tano ndio husimama na kuwa biashara bora ndani ya miaka mitano!!
Sasa kwa nini nasema ujipange sawasawa?
Nasisitiza kwamba ujipange sawasawa ili usije kujitoa kwenye msafara wa wana mafankio. Wengi sana hupenda kuingia katika msafara huu. Lakini wachache sana huweza kuendelea na safari. Ndio maana wahenga wakasema “ kwenye msafara wa mamba na kenge wamo “. Sasa kenge ndo akina nani?
Kenge ni wale ambao wako tayari kujitoa mda wowote kwenye msafara wa safari.
Nifanyeje ili niweze kujipanga sawasawa?
Weka malengo. Unahitaji kuwa na malengo makubwa ambayo yatakupa msukumo katika kufanya kazi yako na kufikia mafanikio.
Ntafaidikaje kwa kujipanga sawasawa?
Kujipanga sawasawa kutasaidia
- Kukamilisha malengo ambayo umekwisha jiwekea.
- Kutokata tamaa wakati
- Kukabiliana na kila aina ya changamoto