Unahitaji Kufanya Haya Kila siku.


Katika safari ya kuekekea mafanikio kuna mambo ambayo unahitaji kufanya kila siku ili uweze kufikia kila siku kwenye njia ya mafanikio.
Mambo hayo nitayaekekeza hapa chini kama ifuatavyo.

1. Kusoma vitabu.
Siku bila kusoma lazima ujisikie mnyonge. Hii ni kwa sababu unakosa maarifa mengi sana kutokana na kutosoma vitabu. Ili tuweze kukuza maarifa ya akili zetu tunahitaji kuwa tumesoma vitabu vingi sana. Je wewe uko tayari kuyakosa maarifa haya?
Ebu jisemee maneno haya kila siku ” siku bila kusoma kitabu hunifanya mnyonge”
Anza sasa kusoma vitabu bila kuchoka.

2. Kuweka alama.
Kila siku hakikisha unafanya kitu ambacho kitaongeza thamani kwenye maisha ya mtu. Watalaam wanasema hujaishi leo kama hujaweka alama. Je wewe umeweka alama gani leo? Je, umefanya nini cha kuongeza thamani kwenye maisha ya watu? Huhitaji kuwa na kundi kubwa la watu ili uweze kuanza kutoa thamani. Anza na hao wachache ulionao.

3. Kuwa mzuri
Je kuna shughuli au kazi ambayo unaifanya ambayo ina mchango mkubwa sana kwa watu?Je,  shughuli unayoifanya unaifanya kwa kiwango kikubwa unachotegemewa kufanya? Je, unampenda kila mtu bila masharti? Je, unawajali wengine? Je, unatoa bika kutegemwa kupokea?  Je, unawajali wengine?
Hayo ndio maswali ya msingi ya kujiuliza kila siku ili ujue kama wewe ni mzuri au la! Kama maswali yote yalivyo hapo juu yanaonesha kwamba uzuri unaozungumziwa hapa sio urembo, utanashati  n.k
Uzuri unaozungumziwa unalenga kwenye  thamani unayotoa kwa watu wengine.

4. Kulala na kuamka mapema.
Unahitaji kulala na kuamka mapema kila siku. Kulala mapema na kuamka mapema kutakufanya mtu mwenye furaha na afya tele. Lakini pia utapata nafasi ya kituafakari maisha yako pamoja na kupata mda wa ziada.

Haya ni mambo ya msingi ambayo kila mmoja wetuanapaswa luyaganya kila siku ili kuweza kufikia hatua kubwa kimaendeleo.

Endelea kutembelea blogu hii kwa makala zaidi za kuelimisja na kuhamasisha kila siku.


Gofius Rweyongeza
Tuwsiliane
godius rweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asannte.

Unaweza kuupenda ukurasa wangu wa facebook kupitia.  fb.me/songambeleblog


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X