Je, umeshawahi kufikria juu ya kuwa na biashara yako mwenyewe. Je, unajua ni faida gani utazipata pale utakapokuwa na biashara yako mwenyewe?
Karibu ndugu msomaji wa songa mbele blog ili kwa pamoja tuweze kujifunza faida utakazozipata pale utakapokuwa na biashara yako mwenyewe.
1. Wewe ndio mwongozaji
Unapokuwa na biashara zako wewe ndio unakuwa kiongozi wa biashara yako mwenyewe. Unaepukana na kuongozwa na kupelekwa usipopataka. Wewe ndiye utakayepanga ufanye nini na kwa mda gani? Japokuwa tu utahitaji kusikiliza maoni ya wateja na waajiriwa wako ila sio kwamba lazima utafuata kile wanachokisema.
2. Unakuwa na nafasi ya kufikia ndoto yako.
Je, umewahi kufikiri nani alianzisha mtandao wa facebook na kuujenga mpaka ukawepo? Au umewahi kufikiri nani alianzisha nguo unazovaa mpaka sasa zipo? Hayo yote na mengine mengi yalikuwa mawazo na ndoto za watu. Je wewe una ndoto yako ambayo ungependa kuifikia? Anza sasa ili na wewe uweze kuifikia ndoto yako. Inapendeza sana pale utakapoona ndoto yako inasaidia watu wengine na wananufaika kutokana na wazo lako.
3. Unapata kuwasaidia watu.
Je, umewahi kufanya kitu ambacho kinasaidia watu? Utajisikiaje pale bidhaa yako itakapokuwa msaada mkubwa kwa watu?
Ingawa biashara siku zote hulenga kupata faida lakini huwezi kupata faida kama wewe hujatoa huduma kwa watu. Ukiwasaidia watu kwa huduma yako na wewe unafaidika. Kwa hiyo watu watapata nafasi ya kuifurahia huduma yako na wewe utapata faida. Ebu chukulia mfano wa Bakhresa huyu amewasidia watu kwa kusogeza huduma mbalimbali kama vile juisi n.k
Watu wanaifurahia huduma yake na yeye anazidi kuwahusumia zaidi huku akitengeneza faida.
Na wewe unaweza kuwa mmoja wao fikri sasa ni jambo gani unaweza kulifanya ili uwasaidie watu.
4. Unaweza kupata muda zaidi
Utakapokuwa na biashara zako kuna uwezekano mkubwa sana wa wewe kuwa na mda mwingi kukaa na ndugu zako, uwapendao, na kuendeleza biashara nyingine.
5.Utaamua umwajiri nani?
Unapokuwa na biashara yako utaamua ufanye na nani kazi au usifanye na nani. Hii ni tofauti kabisa na pale unapokuwa umeajiriwa. Kwa sababu muda mwingine utakazimika kufanya kazi na watu usiowapenda, na kufanya kazi usizozipenda na muda mwingine kufanya kazi siku usizopend kama vile siku za mwisho wa wiki.
6. Unaweza kutengeneza hela zaidi.
Lengo kubwa la kuanzisha biashara ni kutengeneza pesa zaidi ili uweze kuwa huru kiuchumi. Biashara yako inaweza kukuweka huru kiuchumi na kukupa kipato ambacho hata huwezi kukipata kama utakuwa umeajiriwa.
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848381
Asante.
Unaweza kuupenda ukurasa wangu qa facebook kupitia fb.me/songambeleblog