Zifahamu Sheria za Asili za Kuwa Tajiri


Katika maisha ya kawaida kuna sheria nyingi zimetuzunguka na inabidi tuzifuate. Katika mazingira yetu kuna sheria za serikali za mitaa, sheria za serikali kuu na pengine sheria za kimataifa. Zote hizi huwa inabidi zifuatwe na ikitokea umezivunja basi kuadhibiwa huwa kunafuata. Adhabu hutolewa kulingana nabsheria ulizozivunja.

Vilevile sheria za asili zimekuwepo zipo na zitaendelea kuwepo. Mfano wa sheria za asili ni ile sheria ya uvutano ya Newton. Hii sheria sio kwamba ilianza kuwepo baada ya kugunduliwa na Newton bali ilikuwepo hata kabla Newton hajazaliwa.
Vivyo hivyo kwa sheria za asili za kuwa tajiri. Sheria hizi zimekuwepo tangu kuumbwa kwa dunia. Wale watu walioweza kuendana na sheria hizi hata kama hawakujua waliweza kufanikiwa lakini wale waliopingana nazo hawakuweza.
Hizi hapa ni baadhi ya sheria za asili.

1.  Nunua raslimali.
Raslimali ni kitu kinachokuingizia pesa. Kadri unavyokuwa na raslimali nyingi ndivyo unavyokuwa na vyanzo vingi vya kukuingizia pesa. Na ndivyo unavyoweza kuingiza pesa nyingi zaidi.

2.  Weka  asilimia  kumi (10%) kama akiba 
Katika kila hela unayoingiza katika mfuko wako kwenye sehemu ya kipato, toa asilimia kumi au zaidi kwa ajili ya akiba  ya baadae.

3. Tumia pesa ikutengenezee pesa zaidi.
Katika sheria namba mbili tuliona kwamba yatupasa kuweka akiba. Sasa hiyo akiba uliyoipata kwenye namba mbili itumie kununua raslimali zaidi au kuwekeza.
Utagundua kwamba mzunguko unaanza kujirudia tena.

Hizo ndizo sheria ambazo mababu zetu waliokuwa matajiri walizifuata, matajiri wa sasa wanazifuata, na wewe pia zifuate.
Ni rahisi sana ukiamua kutengeneza pesa lakini ni vigumu sana  pale unapoamua kutotengeneza pesa.
Nakushauri uanze sasa maana hakuna wakati mwingine kama  sasa. Amua sasa na  badilika sasa

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kila siku kutoka kwenye blogu hii.


fb.me/songambeleblog


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X