Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG. Ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua za kuelekea na kufikia mafanikio. Karibu sana kwenye makala yetu ya leo.

Jana nilikuwa nasoma kitabu cha FROM VICTIM TO VICTOR ambacho kimeandikwa na mwandishi Joseph Chabalika Mushalika. Kuna mambo mengi sana nimepata kujifunza ila kwa leo ningependa kukushirikisha sentensi moja ambayo binafsi baada ya kuisoma ilinifanya nicheke . Kabla sijakwambia sentensi yenyewe ni ipi ningeomba nikuuliize maswali machache. Hivi ukipata mda wa ziada kwenye maisha yako utaufanyia nini?  Kama wewe ni mwanafunzi ukipata likizo utaifanyia nini? Kama wewe umeajiriwa au umejiajiri ukipata likizo utaifanyia nini? Bila shaka kila mtu ana jibu lake. Inashangaza sana ukiwauliza wengi maswali hayo watakupa majibu mengi sana huku asilimia chache ya majibu yakiwa mazuri sana na mengine yakiwa ya yanashangaza kabisa.

Mwandishi Joseph Chabalika Mushalika anasema kwamba watu hawatumii muda wao vizuri. Anaendelea kusema kwamba “kuna baadhi ya familia kuna mashindano ya kusinzia muda mrefu sana” hii sentensi ilichekesha lakini pia ilinishangaza. Yaani badala ya mtu kuangalia muda mchache alionao autumieje anaangalia aupotezeje? Hivi kweli huyu mtu yuko makini.  Matokeo ya jambo kama hili yanawezekana yasionekane ndani ya muda mfupi lakini baada ya muda mrefu yakajitokeza. Yawezekana leo unalipwa na una mshahara mzuri lakini itafikia hatua hakuna mshahara na pensheni imeisha  sasa sijui utafanyaje.

Kuna msemo mmoja wa kiingereza huwa napenda sana kuutumia, msemo unasema hivi “ early to bed , early to rise makes a person healthy,wealthy and wise”  yaani kulala mapema na kuamka mapema kunamfanya mtu anakuwa mwenye afya, tajiri, na mwenye busara.
Kulala lini? Mapema. Hakuna utani! Na kuamka lini? Mapema! Hakuna utani!  Hakuna mtu ambaye anasifia uzembe hata kidogo. Hata kitabu cha biblia katika mithali 6:6-11 kinasema 

Ewe mvivu mwendee chungu zitafakari njia zake ukapate hekima.

Kwa maana yeye hana akida wala msimamizi wala mkuu. 

Lakini hujiwekea hatua ya chakula wakati wa jua. Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno

Ewe mvivu utalala mpaka lini? Utaondoka lini kwenye usingizi wako? 


Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo.

Bado kukunja mikono ili upate usingizi.

Hivyo umaskini wako huja kama mnyanganyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.



Katika kifungu hicho kuna mambo mengi sana ya kujifunza ila kwa sasa naomba tuangalie hiyo sentensi inayosema  “ewe mvivu utalala mpaka lini”?
“Utaondoka lini kwenye usingizi wako”?

Nakumbuka mwanzoni mwa makala hii nilikuuliza swali “hivi ukipata mda wa ziada utaufanyia nini”?  Ikitokea ukapata likizo kama wewe ni mwanafunzi au umeajiriwa au vinginevyo utaitumia kufanya nini?

Najua kila mmoja atakuwa na jibu lake linalohusu swali hili?

Sasa hapa nakupa mambo mawili ambayo unaweza kuyafanya kwa kuutumia juu ya  muda wako.

1.Wekeza katika muda.
Anza sasa kuutumia muda vizuri, kwa kufanya mambo ambayo yatakuja kukusaidia baadae.

Kama wewe ni mwanafunzi soma sasa na matokeo yake utayona baadae

Kama wewe ni mkulima lima sasa kitaalamu  na kwa kufuata mbinu za kisasa na uzalishe mazao bora na matokeo yake utayaona baade.

Kama wewe umeajiriwa fanya kazi vizuri sana na kwa moyo wako wote  na matokeo yake utayaona baade.

Kama wewe ni mfanya biashara toa huduma nzuri na inayopendeza kwa wateja wako na matokeo utayaona baadae

Kama wewe unataka kuwa mwandishi andika sasa kwa kutoa thamani na matokeo yake utayaona baadae

Kama wewe hujui cha kufanya anza kusoma vitabu sasa na matokeo yake utayaona baadae

Soma zaidi hapa; Vitabu Vitatu Vya Kusoma Kabla Mwaka Huu Haujaisha

Faida Sita (06) za kusoma Vitabu Na Makala Za Kuelimisha

2. Kuupoteza muda
Kama utashindwa kuwekeza katika mda amua kinyume chake. Amua sasa kuupoteza muda kwa kulala na matokeo yake utayaona baadae.

Kama wewe ni mwanafunzi amua sasa kutosoma na kuzurura mitaani na matokeo yake utayaona baadae

Kama wewe ni mkulima amua sasa kutolima, au lima bila kufuata kanuni za kilimo na matokeo yake utayaona baadae

Kama wewe umeajiriwa amua sasa kuanza kuchelewa kazini na kufanya kazi kwa uzembe na matokeo yake utayaona baadae

Kama wewe ni mfanyabiashara amua sasa kuanza kuwadanganya wateja wako kuhusu bidhaa unazotoa na matokeo yake utayaona baadae

Soma zaidi hapa; Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo

Nashauri kila mtu awekeze katika muda kuliko kupoteza muda maana kupoteza muda ni hatari sana.
Je wewe unaamua kufanya nini?

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Kujiunga na mfumo maalumu wa kupokea makala maalumu kutoka songambele BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA UJAZE FOMU

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X