Habari za leo rafiki na ndugu yangu, ni imani yangu unaendelea vyema ili kufikia mafanikio na kuwa na maisha bora. Karibu sana katika makala yetu ya leo.
Leo tunaenda kuona duka lako lenye kila kitu. Duka hili unaweza kulitumia kila siku popote pale ulipo na kukusaidia kufikia hatua kubwa ya mafanikio.
Soma zaidi hapa: Hii Ndiyo Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo
Je, duka lenyewe ni lipi?
Kufikiri ni duka kubwa sana ambamo mawazo yanapewa umbo, mwonekano na kuwekwa katika matendo.
Kupitia kufikiri mwanadamu ameweza kutengeneza mambo makubwa sana kwa karne moja iliyopita. Kuliko ambavyo aliwahi kufanya kwa kwa karne zilizopita. Ameweza kukadria umabali kutoka kwenye dunia hadi kwenye jua, lakini pia ameweza kujua ni vitu gani vinaunda jua. Amegundua kwamba ubongo wake ni kisima kizuri sana na anaweza kufanya mambo makubwa sana kwa kutumia ubongo wake.
Ameweza.kugundua televisheni ambazo zinarusha matangazo kwa njia ya picha. Lakini kikubwa zaidi ameweza kutengeza simu za kisasa na kompyuta ambazo zimeleta mabadilikobmakubwa sana katika historia ya binadamu na kutuingiza katika zama nyingine.
Yaani kikomo cha kufikiri kimo ndani ya binadamu mwenyewe.
Kuna vitengo viwili vya kufikiri.
1. Kufikiri kwa awali
Kupitia kufikiri kwa aina hii mtu anaweza kufikiri na kupangilia mipango ya zamani na kuiboresha kuwa bora zaidi. Mipango hii inawezekana aliiweka mwenyewe au iliwekwa na watu wengine. Anaweza kuiboresha na kuiongezea thamani zaidi. Kitengo hiki kinashughulika na mambo ambayo kimeona, kimesikia au kimefundishwa. Kitumie vizuri kitengo hiki maana unacho tayari katika akili yako.
2 Kufikiri kwa ubunifu
Katika kitengo hiki ndipo msukumo wa kufanya jambo fulani jipya hutokea. Kupitia hapa matakwa yote, habari mpya na mawazo mapya humfikia binadamu. Ni katika kitengo hiki unaweza kugundua mambo mapya.
Vitumie vitengo hivi ili uweze kufaidika navyo. Umezaliwa navyo wala huitaji kuvinunua dukani . unaweza kuvitumia mda wowote na saa yoyote ila mda wa kuanza ni sasa.
Tuwasiliane Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante