Hili Ni Jambo Linalokuzuia Kufika Unapotaka


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo.

Sio jambo la kushangaza sana kusikia mtu anasema “amekwama”. Mtu aliyekwama anapoteza mwelekeo, yupo njia panda na hajui afanye nini? Je wewe umewahi kuwa katika hali kama hii? Macho yote yamekuangalia lakini hukujua ufanye nini? Kuna watu katika hali kama hizi wanapoteza mwelekeo na kuanza kuvuta sigara, kunywa pombe na mengine mengi.

Je hali kama hii husababishwa na nini? Yapo mambo mengi sana yanayosababisha hali kama hii kakini kwa leo ningependa kukushirikisha moja tu. Tufuatane mapaka mwisho ili tuweze kuielewa zaidi.

Soma zaidi; Ufahamu Uovu Wa Lazima Kwenye Maisha Yak
Kuridhika na kutulia
Je kuna shida gani katika kuridhika? Unaweza kuuliza hivyo. Kuridhika ni kuwa na furaha na amani juu kitu au hali fulani. Ni vizuri sana kuridhika lakini haifai hata kidogo kama maisha yako ni hali ya chini. Unaweza kuridhika wakati hauna uwezo wa kununua matumuzi ya ziada kwa familia yako? Unawezaje kuridhika wakati watoto wako wanagombania karo ya shule ? Unawezaje kuridhika wakati huna hata uwezo wa kumsaidia mtu maskini mmoja?

Kadri siku zinavyokwenda  ndivyo watu wanavyozoea hali fulani ya na kuifanya kuwa sehemu ya maisha yao. Ile hamu ya kutafuta maisha bora hupotea na kujikuta wameridhika huku wakiwa hawana kitu. Kiukweli kwa namna hii kuridhika hakupaswi kuvumiliwa

Hakuna mwanadamu ambaye amekuja hapa duniani kutulia na kuangalia mambo yanavyokwenda. Kutulia kunaua kufikiri na kukufanya uwepo badala ya kuishi. Unakuwa maada ( chochote chenye uzito na kinachukua nafasi). Hata dunia yenyewe siku zote ipo kwenye mwendo. Siku zote dunia ipo inajizungusha yenyewe kwenye mhimili wake, lakini pia inalizunguka jua. Ni kutokana  na kuzunguka kwa dunia tunapata  usiku na mchana, pamoja na majira ya mwaka. Lakini pia tunavutwa kwenye kiini cha dunia. Dunia imeanza mizunguko yote hii miwili tangu kuumbwa kwake na bado inaendelea kuzunguka kila siku. Haijawahi kuamua kusema sasa nimeridhika ngoja nitulie niache kuzunguka.Hivi itakuwaje pale ambapo dunia itaacha kuzunguka? Maisha hakuna duniani. 

Soma zaidi hapa; Utavuna Ulichopanda; Hii Ndiyo Sheria Kuu Ya Asili

Kwa nini sasa wewe unaridhika na kutulia? Sasa kwa nini wewe unataka kuacha kusongambele Utaendelea kuilalamimkia serikali mpaka lini? Raisi wa marekani John Kenedy aliwahi kusema “usiulize marekani imekufanyia nini jiulize umeifanyia nini marekani?  Ebu na wewe usikae tu na kutulia ukiwa unasubiri serikali ikupe hela. Au usitegemee serikali ije ikupe soko wakati hata huwezi kuzalisha chakula cha kuitosha familia yako. Mambo ya kwenda kijiweni na kuanza kuilalamimkia serikali kwamba haifanyi vizuri unapoteza muda. Kwa nini huo muda wa kulalamika usiutumie kufanya jambo lako la ziada. Kumbuka hata ukiwa muongeaji kiasi gani kijiweni kwako hakuna kitu utakachokibadilisha kwa serikali. Lakini kuna mtu mmoja unaweza kumbadilisha na mtu huyo ni wewe. Je wewe serikali umeifanyia nini?

Soma zaidi hapa; Hii Ndiyo Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo 

Usikae tu na kuridhika chukua hatua.

Kutulia ni moja ya matokeo ya kuridhika. Kama tulivyoona hapo juu kwamba kuna hatari sana katika kutulia. Ebu tuone mambo ambayo yanaweza kujitokeza katika kutulia kwa kuangalia mifano hii.
Mbu wanaoeneza malaria huzaliana
 katika maji ya utulivu na ni hatari sana. Konokono wanaoeneza kichocho hupatikana katika maji ya utulivu na  kichocho ni hatar sana. Hee! Kumbe kumbe kuna hatari sana katika utulivu ebu tuwe watu wa kusongambele kila wakati.
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii. 
Kujiunga na mfumo maarumu wa kupokea makala kutoka songambele  BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA UJAZE FOMU
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Godius Rweyongeza
Tuwasiluane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X