Huu Ni Ugonjwa Hatari Unaokusumba Sana


Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa mtandao wa SONGA MBELE. Ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kufikia malengo yako na mafanikio. Karibu sana katika makala yangu ya leo

Kuna ugonjwa mmoja ambao huwa unasumbua watu wengi sana. Ukiongea na watu kumi basi utagundua kati ya hao kumi, saba mpaka tisa wana ugonjwa huu.

Ugonjwa huu ni wa hatari sana kama yalivyo magonjwa mengine kama vile Malaria. Lakini ubora wa ugonjwa huu ni kwamba unatibika na tiba ya ugonjwa huu unayo wewe mwenyewe.

Je ugonjwa huo ni upi?
Huu ni ugonjwa wa udhuru.

Ukifuatilia kwa umakini kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafikia mafanikio utagundua tofauti kubwa iliyopo ni udhuru.

Watu waliofanikiwa sio kwamba hawawezi kutoa udhuru za kwa nini  wasifanye jambo fulani. Lakini wameamua kuziweka pembeni baada ya kugundua kwamba udhuru hazileti mafanikio.

Mwalimu nyerere, angeweza kusema mimi ni mtoto kutoka katika familia maskini na isitoshe mimi ni mwalimu, sina ujuzi wowote kuhusu siasa kwa hiyo siwezi kuikomboa nchi. UDHURU.

Diamond angeweza kusema mimi nimetoka kijijini kabisa ngoja kuimba niwaachie wajanja wa mjini.

Kumbe sio hivyo. Wewe una kitu ndani yako ambacho hujaanza kukifanyia kazi. Wewe ndiye mjanja nambari moja katika dunia hii.

Sasa kwa nini wewe unakuwa na udhuru nyingi sana? Mara utasikia mtu anasema eti mimi ni mgonjwa au mlemavu kwa hiyo siwezi kujishughulisha na kitu chochote. Mbona kunawatu wengi sana kama wewe lakini bado wanafanya kazi na kuingiza kipato kikubwa sana.

Mwingine atasema mimi ni mzee au mtoto.
Lakini kuna ambao wamepata mafanikio wakiwa wazee. Hii inaonesha ni kwa kwa namna gani mafanikio yanaweza kupatikana popote.

Kuna watu wenye umri mdogo sana  kama Justin Bieber ameweza kufikia mafanikio katika umri wake mdogo. Na kuna watu wenye umri mkubwa na wao pia wameweza kufikia mafanikio makubwa Je wewe unasubiri nini? Kama hawa wameweza kwa nini wewe usiweze.

Najua zipo udhuru nyingi sana ambazo mtu  unaweza kuwa nazo. Hizo nimeandiaka baadhi kama na wewe una tatizo au kitu ambacho unafikiri kinakukwamisha kiweke kwenye sehemu ya maoni na kitajibiwa haraka sana.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya kuondokana na ugonjwa huu.

1.Fikria chanya. Chukua mda wako kuona vitu katika uchanya wake na ubora wake. Usilalamike kwa kila kinachokuja mbele yako bali kione kama fursa ya wewe kusonga mbele.

2 Kaa na watu wenye mtazamo chanya.
Najua unao marafiki zako wengi sana. Ebu angalia kati ya hao ni wapi watakufaa wewe kufikia mafanikio yako. Ni watu gani utakaa nao wanaofurahia maisha yao mda wowote. Watu wenye ujasiri wa kubadili maisha yao na kusongambele. Furahia kila dakika ya maisha yako.

3. Ijue thamani ya muda
Fahamu kwamba kila mtu anyo masaa 24 kwa siku. Utumie mda wako vizuri. Usianze siku mpya bila mpango na usimalize siku bila kuifanyia tathmini. Ni vizuri sana kufahamu umuhimu wa muda



4. Ishi leo.
Hivi kama ungeambiwa leo ni siku yako ya mwisho ya wewe kuishi duniani ungefanyaje.
Siku zote watu wamekuwa wakiishi  siku nyigine zote lakini wanashindwa kuishi leo. Furahia kila dakika katika kila kitu unachofanya. Fanya kile unachopaswa kukifanya na kifanye kwa ubora zaidi.

Nakutakia safari njema ya kuelekea mafanikio.

Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu za kila wiki BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye  blogu hii.

Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
07558848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X