Je, Kupenda Pesa Ni Chanzo Cha Maovu?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blog ya SONGAMBELE; karibu sana katika Makala yetu ya leo ambapo tunaenda kuona kama kupenda pesa ni chanzo cha maovu. Hapa tutaona vipengele muhimu vinavyotuonesha kuhusu kile tunachoenda kujadiliana.

Wiki iliyopita tulijadili kuhusu suala zima la pesa ni nini?  Kama hukusoma Makala ya wiki iliyopita unaweza kubonyeza hapa kuisoma maana Makala ya leo ni mwendelezo wa Makala ya wiki iliyopita

kwa wale ambao Biblia ni chanzo chao cha maarifa kuna mambo mengi sana yameandikwa kuhusu pesa ambayo pia yanaweza kumsaidia mtu yeyote. Kuna baadhi  ya watu wanasisitiza wenzao kuikimbia pesa wakati wengine wanasisitiza wenzao kuelewa kanuni za pesa na kuifanya pesa iwafanyie kazi. Wakati kuna baadhi ya familia ambazo kwao kuzungumzia pesa mezani ni marufuku wakati huo huo wanawasisitizia watoto wao wao wasome wapate elimu nzuri ili wakaajiriwe kwenye kampuni zuri na inayolipa vizuri, inashangaza kidogo kuona wazazi ambao wanawakataza watoto wao kuzungumzia masuala ya pesa mezani hao hao wanwasisitiza wasome wakaajiriwe ili wapate mshahara mzuri.

Tukirudi kwenye kwenye mada yetu ya leo, je, kupenda pesa ni chanzo cha maovu?  Kama tulivyoona wiki iliyopita kwamba pesa ni kipimo  cha  mafanikio hapa duniani. Kuhusu suala kuwa bwana au mtumwa pesa limeelezwa vizuri sana katika kitabu cha Mathayo 6:24
Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili maana atamchukia huyu na kumpenda huyu, atashikamana na huyu na kumchukia huyu hamwezi kumtumikia Mungu na Mali”

Soma hapo kwa umakini. Nakusihi usome hapo kwa umakini hayo yaliyokazwa. Kila kitu kimewekwa wazi kwamba huwezi kuwa na mabwana wawili,  katika sentensi hiyo tunaonyeshwa ni kwa jinsi gani hatupaswi kuwa watumwa wa pesa bali tunapaswa tuitumie pesa itufanyie kazi.

Katika Makala zangu zote nimekuwa najaribu kuonesha ni kwa jinsi gani unapaswa kuitumia pesa ikufanyie kazi yaani uitumie pesa ikutumikie wewe sio wewe uitumikie pesa.

Kitu ambacho kimeandikwa kwenye mstari hapo juu sio kwamba pesa ni mbaya, tatizo sio pesa, tatizo ni wewe. Kwa hiyo pesa kama zilivyo zawadi nyingine ambazo tumepewa na Mungu hatupaswi kuiabudu pesa, tunapaswa kumwabdu aliyetoa.

Pesa ni mtumwa mzuri sana, inahakikisha ulinzi wa mmiliki, inakufanyia kazi unapokuwa umelala, inaondoa aibu kwa wale ambao tungepaswa  kuwahudumia na kukosa kuwahudumia. Tunaona hadi nchi zenye pesa au wengine wanaziita nchi zilizoendelea ziaziwekea vikwazo nchi maskini. Je, umewahi kusikia nchi maskini imeiwekea nchi tajiri vikwazo?

Je. kuna mtu anafurahi kuona watoto wake wanaachishwa shule kwa sababu ya pesa ?  Je nani atafurahi kuona watoto wake wamevaa matambara na kujifunika shuka moja lilichanika?
ndugu msomaji wa songambele nakualika  uangalie mtazamo wako pesa ukoje.

Kiujumla ni kwamba pesa kama pesa yenyewe sio uovu bali matumizi yako ndio yatatuambia kama pesa ni uovu au la!. Kama utaitumia pesa kufanya mambo mazuri basi pesa ni nzuri. Kuwa na matumizi sahihi ya pesa. Ukiitumia pesa kufanya maovu basi pesa inakuw si jambo zuri tena bali uovu. Je, wewe unaitumiaje pesa yako?

Pesa inaweza kutumika kujenga hospitali, shule, vyuo barabara, kuwalisha watu wasio na chakula. Kama utatumika kufanya mazuri kama haya basi pesa inakuwa ni jambo jema sana. Lakini kama itatumika kufanya mabaya basi sina budi kurudia tena kwamba kwa mantiki hiyo pesa itakuwa chanzo cha maovu.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii

Kujiunga na mfumo wetu wa kutumiwa makala marumu za kila wiki BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA UJAZE FOMU.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X