Matendo Hutibu Uoga


Moja kati ya vitu ambavyo husumbua sana akili za watu ni uoga. Uoga upo na unasumbua san akili za watu uoga unaweza kukufanya ushindwe kuchukua hatua fulani. Uoga ambao watu wengi wanao ni wa kisaikolojia.  Uoga, hofu, mvutano vyote hutoka kwenye mawazo hasi.

Uoga si kitu kizuri cha kukumbatia hata kidogo. Uoga ni adui nambari moja wa wa mafanikio. Uoga utakufanya usishughulike na fursa zinazoweza kujitokeza. Uoga unakuondolea mwaonekano wako wa kawaida, uoga unakupunguzia maisha, uoga unakufunga mdomo unapotaka kuongea, lakini pia uoga huondoa kujiamini. Uoga utakwambia kwa nini watu wengi wameshindwa, utakwambia kwa nini watu wengi wanapata kidogo na kufurahia kidogo. Ama kweli uoga una nguvu kubwa sana.

Ebu tuone mfano huu. James hakuwa na kazi. Alikuwa akihangaika kutafuta kazi kwa siku nyingi, siku moja akisoma gazeti aliona kwamba kuna nafasi ya kazi kwenye kampuni moja kubwa sana. Alianza kuogopa kwamba itakwaje kama ataamua kwenda, kuomba kazi, akaanza kufikria itakuwaje kama atakosa, akaanza kujiona mshindwa. Na mtu ambaye hawezi. Siku moja kabla ya kwenda kuhojiwa na kuchukua vyeti vyake hofu iliongezeka mara dufu. Alichelewa kulala na aliamka asubuhib akiwa amechelewa sana. Katika kuangalia nguo ambazo alipaswa kuvaa akagundua nguo zake hazijafuliwa, akaamua kuvaa nguo ambazo alikuwa hajapanga na zilikuwa hazijanyooshwa. Akavaa hivyo hivyo zimejikunja. Alipofika sehemu ya kuhojiwa alionesha wasiwasi mkubwa na mda wote alikuwa akihofia shati na suruali yake vilivyojikunja. Hii ilimfanya aonekane akiwa hafai.

Anita alienda kuomba kazi hiyohiyo, wiki moja kabla ya kuhojiwa alijiona mshindi tayari. Siku moja kabla yankuhojiwa aliandaa nguo zake zote na kuzipiga pasi. Alilala mapema na siku yenyewe kabisa  akaamka mapema. Alivaa nakuelekea sehemu ya kuhojiwa mapema. Nusu saa kabla ya kuhojiwa alikuwa yupo kwenye eneo husika. Alipoanza kuhojiwa aliongea kwa kujiamini bila uoga wowote. Mwisho wa siku alipata kazi na James alikosa.
Je  tunajifunza nini kutoka nini kutoka kwenye simulizi hii?
Kuna muujiza wowote ulifanyika?
Hapana, kila kitu kilitokea kwa njia ya kaawaida sana.

Je, niafanye nini ili nifanikiwe?

Kuna aina nyingi sana za uoga. Lakini zote unaweza kuzigeuza kuwa kujiamini. Kujiamini si jambo la kuzaliwa nalo wala hakuna mtu ambaye amewahi  kurithi kujiamini. Kujiamini unakutengeneza mwenyewe. Kujua kwamba unaogopa  bila kuweka juhudi za matendo hakuwezi kutibu uoga. Ni sawa na dakitari akigundua kwamba wewe ni mgonjwa haishii tu hapo, bali atachukua hatua kuhakikisha unapona.
Vivyo hivyo kwa uoga.

Kama una uoga kwa sababu ya mwonekano wako. Usiogope. Unaweza kwenda kwa kinyozi kunyoa nywele zako, ukasafisha nguo zako na kuvaa nguo safi. Hii haiitaji kwenda kununua nguo mpya.

Kama unaogopa utampoteza mteja, fanya kazi na toa huduma nzuri, sahihisha kila kitu ambacho kinaweza kusababisha mteja aondoke.

Kama unaogopa kushindwa mtihani, ubadili mda wa kuogopa uwe wa kusoma.

Kama una uoga juu ya kitu ambacho huwezi kukizuia, badilisha umakini wako kwenye kitu kingine kama kufanya kazi unayoipenda au kusoma kitabu  unachokipenda.

Kama unaogopa wengine watasemaje, au watafikiri nini kuhusu wewe. Hakikisha unaweka mipango na kufanya kitu kwa usahihi. Hakuna mtu ambaye huwa anafanya kitu vha tofauti bila kusemwa. Ukiona hujasemwa jua unafanya kitu ambacho kila mtu amaezoea kufanya.

Kama kuna watu unawaogopa, badilisha mtazamo wako. Kumbuka mtu mwingine ni kama wewe.

Soma zaidi hapa: Ifahamu Tofauti Kati Yako Na Huyu

Kama kuna kitu kinakupa uoga au kinakufanya usijisikie vizuri na sijakisema hapo juu usisite kuweka maoni yako hapo chini ili ujibiwe.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii

Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maafumu kila wiki BONYEZA HAPA NA UJAZE FOMU

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X