Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo – 2


Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG, ni imani yangu unaendelea vyema katika harakati za kuelekea mafanikio. Karibu sana katika makala yetu ya leo.  Makala yetu ya leo ni mwendelezo wa makala ya wiki iliyopita, kama hukusoma makala ya wiki iliyopita unaweza kuisoma HAPA

Basi siku zikaendelea na hatimaye mtoto
akapata kazi na kuanza kuuza nyanya kwenye
soko. Mtoto akawa anaingiza pesa nyingi sana.
Baba yake “alipomuuliza unawezaje kuingiza
pesa nyingi kiasi hicho”
Mtoto alisema “Nachukua nyanya nzuri
naziweka chini, mbaya naziweka katikati na
nyingine nzuri naziweka juu.
Baba yake akamwambia “wewe ni mjanja sana
mwanangu”

Basi mtoto aliendelea na ujanja wake na siku moja alikuja kufanya kitendo ambacho kiliwaaibisha sana wazazi na ndipo baba akamwambia mtoto wake mbona umefanya kitendo cha kutuaibisha sisi wazazi wako na wakati sisi tunaheshimika sana hapa mtaani? Ndipo mtoto akamwambia baba yake “unakumbuka siku ile tulipokuwa njiani tunaenda kutembea na ukatoa rushwa baadae ukaniambia kila mtu anafanya hivyo hapa mjini.
Akamwambia mama yake unakumbuka siku ile uliponunua vitu vya elfu tatu nakutoa elfu tano ukarudishiwa shilingi elfu saba. Nilipokuuliza kwa nini umechukua chenji zaidi ya pesa uliyoitoa si uliniambia kila mtu mjini anafanya hivyo.

Ndipo mtoto akasema na mimi nmefanya kile ambacho kinafanywa na kila mtu hapa mjini.

Kutokana na hadithi hii kuna mambo mengi sana ya kujifunza.

1. Mtoto Umleavyo ndivyo akuavyo.
Msingi mzuri wa mtoto unauandaa tangu akiwa mdogo mtoto ukimuandalia mazingira mazuri ya kuwa mtu mzuri na bora baadae ndivyo ambavyo atakuja kuwa, lakini ukimuandalia mazingira ya  kuja kufanya vibaya itakuja kuwa hivyo. Mwandae mtoto kuwa mtu mzuri ambaye atafanya kile anapaswa kufanya. Kukifanya kwa ubora na kwa umakini wa hali ya juu sana.

Soma zaidi hapa; Je, Shule Na Maisha Vinaendana?

2. Uwazi. 
Mfundishe mtoto wako kuwa muwazi na mkweli katika kile ambacho anakifanya. Atajijengea uaminifu wa kudumu. Kama huyu mtoto angekuwa anafanya uaminifu katika biashara yake biashara yake ingedumu kwa mda mrefu sana bila kuteteleka lakini kutokana na ukosefu wa nidhamu kazini unaweza kuona kwamba biashara yake haitafika mbali sana. Hakuna mtu ambaye atawekewa nyanya mbovu katakati na siku nyingine akubali kurudi kununua nyanya zilezile kwa mtu yuleyule. Uaminifu unajenga wateja wa kudumu.

Soma zaidi hapa;  Je, Unaijua Kauli Haribifu Kwenye Maisha Yako

3. Mzazi ni kocha wa mtoto wake.
Kocha ni mtu ambaye anampa mtu mafunzo na kuendelea kumfundisha mpaka anaingia kwenye uwanja wa mapambano. Kocha anaendelea kumfundisha mpaka pale atakapohakikisha amepata mafanikio. Kwa hiyo mzazi  kama atamfundisha mtoto wake  mambo mema basi huyo mtoto atayachukua hayo. Lakini kumbuka yale unayomfundisha sasa itakuwa vigumu sana baadae kuja kuyabadilisha. Kumbe mda wa kumfundisha mambo mema ni sasa.

Kuna mambo mengi sana tunaweza kujifunza kutoka kwenye stori hii karibu naomba tuyatafakari hayo kwa leo.
Unaweza pia kuandika kitu ambacho umejifunza kwenye sehemu ya maoni hapa chini.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutika kwenye blogu hii

Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makaa maarumu za kila wiki kutoka SONGAMBELEBLOG BONYEZA HAPA UJAZE FOMU ILI KUJIUNGA



Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
gidiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante.
Je, Unaijua Kauli Haribifu Kwenye Maisha Ya


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X