Niambie Rafiki Zako Nikwambie Tabia Zako


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG. Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo.

Hivi umewahi kufikiri ulimwengu bila marafiki utakuwaje? Bila shaka ungekuwa mbaya sana!! Moja sifa ya binadamu ni kujamiiana na watu na kutengeneza marafiki. Katika suala zima la kupata marafiki mwanadamu amepiga hatua kubwa sana. Kwa sasa unaweza kuwa na rafiki kutoka nchi yoyote ile duniani. Yaani uwepo wa mitandao ya kijamii umemfanya mwanadamu kufahamia na watu wengi  zaidi. Kiukweli haya mapinduzi hayapaswi kupuuzwa na mtu yeyote.

Soma zaidi hapa; Hili Ni Kosa Ambalo Watumiaji Wengi Wa Mitandao Hufanya

Kadri tunavyizidi kukutana na kufahamiana na watu mbalimbali ndivyo tunavyozidi kukutana na tabia mbalimbali huku kila mtu akiwa na falsafa zake, mtizamo wake, na malengo yake. Kumbe sio rahisi kushirikiana na kila mtu katika suala zima la kuelekea ndoto zako kutokana na kutofautiana katika falsafa, mawazo,malengo, na mtizamo.

Kwa siku nyingi sana nimekuwa nikiona wanafunzi wakitembea katika makundi. Utakuta wanakula pamoja, wanakaa pamoja, mmoja wao akikosa mwingine anakuwa na taarifa za mwenzake kaenda wapi?
Ukifuatilia tabia zao utagundua kwamba kuna kitu wanapendelea kwa pamoja kama kucheza au kushabikia mpira, mziki, filamu,wanasoma pamoja, wanatoroka pamoja, hujificha kazi kwa pamoja, siasa, kusoma vitabu na mengine mengi sana.
Niambie marafiki zako nikwambie tabia zako!!!

Je wewe marafiki zako ni wapi?
Suala zima la urafiki ni kubwa sana tena la kuangalia kwa umakini wa hali ya juu sana. Kama vile chuma kinavyohitaji chuma kingine kukinoa vivyo hivyo wewe unahitaji marafiki  wa tabia hizohizo kama za kwako wakuzunguke.

Mara nyingi sana watu huwa tunaenda kwenye vioo kujiangalia na kuona mwonekano wetu.
Mwonekano wa marafiki ndio utakaoniambia tabia zako ni zipi. Kama utazungukwa na watu wanaokuvuta chini lazima tu utaanguka lakini kama utazungukwa na watu wanaotaka kupanda juu upo njiani kuelekea mafanikio.
Linapokuja suala zima la marafiki chagua.
Chagua marafiki watakaokufikisha kwenye ile sehemu unayotaka kufika.
Niambie marafiki zako nikwambie tabia zako!!!

Mara nyingi sana nmesikia watu wazima wakisema kauli ambazo binafsi huwa sikubaliani nazo.
Unakuta anaanza kukwambia eti “unamwona mtu fulani? Mimi nmesoma naye shule moja darasa moja na chuo kimoja lakini sasa ana vitu kadha wa kadha” hii  kauli mara nyingi watu huitumia pale wanapokuwa wanaongelea watu wanaowafahamu ila wamewazidi kimafanikio. Binafsi huwa huwa nawasikiliza kwa umakini lakini moyoni huwa nina maswali mengi sana ya kuwauliza lakini huwa naacha kuyauliza kwa sababu ya kuwatunzia heshima tu. Je, hawa wenzako walipokuwa wanatafuta mafanikio yao wewe ulikuwa wapi? Ina maana ulikuwa umelala?

Soma zaidi hapa; Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha

Kiukweli wewe ndugu msomaji sitakuonea aibu lazima nikuulize, je, wenzako wanapotafuta maendeleo wewe unafanya nini?
Je, marafiki zako wanakupeleka kwenye maendeleo au wanakurudisha nyuma.
Niambie marafiki zako nikwambie tabua zako!!!
Tafakari chukua hatua.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii

Ili kupata makala maalumu kutoka songambele BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA UJAZE FOMU

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X