Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG. Imani yangu unaendelea vyema katika hatua kuelekea na kufikia mafaninkio. Karibu sana katika makala yetu ya leo.
Hadhi ni nafasi ambayo mtu anayo. Katika makala ya leo tutajikita katika hadhi ya kijamii. Hadhi ya kijamii ni nafasi ambayo mtu anayo katika jamii. Mfano Yakobo an miaka 36 ni mwanaume wa kitanzania, amezaliwa katika familia ya kitajiri yenye biashara mbalimbali, ingawa baba yake Yakobo amesoma sheria na mama yake ni mhasibu.
Yakobo siku zote alijua anataka kuwa mwalimu. Alipofikisha miaka 32, Yakobo alihitimu masomo ya ualimu na kuanza kufundisha katika sekondari ya Mkwawa. Mwaka mmoja baadae Yakobo alimwoa Anitha mpenzi wake wa siku nyingi, baadae yakobo na Anitha mpenzi wake walipata watoto mapacha. Hii ilimfanya Yakobo kuwa na Heshima kubwa lakini wazazi walijigamba zaidi.
Soma zaidi hapa: Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo
Tukiangalia hapo tutagundua Yakobo ana hadhi na vyeo vingi mbavyo ni baba, mume wa mtu, mwalimu, mtanzania na mtoto.
Kuna baadhi ya vyeo au hadhi ambazo mtu anakuwa navyo vinamfanya aheshimike na vingine vinamfanya adharauliwe. Kwa mfano madakatari wanaheshimika sana katika jamii zetu na mhalifu ana dharaulika sana.
Hadhi ya kufikiwa
Hii ni nafasi ambayo mtu hufikia baada ya kufanya kazi kubwa kutegemea na uwezo wa mtu. Hadhi ya kufikiwa kwa maamuzi ya mtu. Mfano Yakobo amefikia hadhi ya ualimu na kuwa mume wa mtu ambazo zote ni hadhi za kufikiwa.Hadhi za kufikiwa zinaweza kuwekwa katika makundi yafuatayo:
- Hadhi inayotokana na vitu unavyomiliki mfano mwenye nyumba, mwwnye garin n.k
- Hadhi inayotokanana cheo mfano daktari, mwalimu,
- Hadhi za kisiasa mfano raisi, waziri mkuu, waziri
- Hadhi kutokana na Mambo uliyofikia mfano mwanamziki , mwanamichezo
Soma zaidi hapa; Hii Ndiyo Maabara Ambayo Kila Mtu Anayo
Hadhi ya kuzaliwa
Hii ni hadhi ambayo mtu hupolea bila kuitaka u kwa kuzaliwa nayo. Mfano Yakobo hakuchagua kuzaliwa na wazazi matajiri. Yote hayo matatu anayapata kwa kuzaliwa nayo tu. Watoto wake walizaliwa mapacha na hilo nalo halikuwa uwezo wake.
- Hadhi inayotokana na jinsia mfano mwanaume au mwanamke.
- Hadhi inayotokana utofauti wa umri mfano
- Zinazotokana na ukoo mfano mtoto wa kiume, mtoto wa kike, dada, kaka, mjomba, shangazi, n.k
Hadhi ya umri
Hii ni hadhi ambayo mtu huipata kulingana na umri wake. Mfano Yakobo ana miaka 36, au mzee au kijana , mtoto, mtu mzima n.k
Endelea kusoma makala za kuelimisha kuyokakwenye blogu hii
Ili upate makala maarumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.
3 responses to “Je, hadhi ni nini?”
Safii
Safii
Pamoja sana ndugu yangu
#UDOSUMU