Je, Unachofanya Kinasaidia Nini?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG. Imani yangu unaendelea vyema katika hatua kuelekea na kufikia mafaninkio. Karibu sana katika makala yetu ya leo.

Ni kawaida sana kwamba watu wamekuwa na mambo mengi sana ya kufanya kwa siku, ukiaangalia mambo  wayonayofanya kwa siku yanaonekanakuwa mengi kiasi kwamba muda wao unaonekana umebana sana. Lakini kitu cha msingi sana cha kufahamu ni kwamba kila mtu ana masaa 24 kwa siku imekuwa hivi kwa siku nyingi, iko hivi, na imani yangu itaendelea kuwa hivi kwa muda mrefu sana. Sina uhakika kama itagundulika njia ya nzuri ya kuongeza muda kwa siku za hivi karibuni. Kumbe kwa pamoja waliofanikiwa wasiofanikiwa tuna masaa 24. Je, wewe unautumiaje muda wako? 

Kwa leo ningependa kujua  muda wako unautumia kufanya nini?
Naamini una mambo mengi sana lakini mambo yote kiujumla nayaweka sehemu tatu tu, kama kile unachofanya hakiendani na n haya kitafakari tena. Narudia tena mambo yote unayofanya hakikisha yapo katika sehemu kuu tatu kama hayaingii kwenye sehemu mojawapo kati ya haya kitafakari tena.

1). Kinakuingizia pesa.
 2). Kinaongeza maarifa
3). Kinaboresha mahusiano

Haya ndiyo matokeo ya mambo kile unachokifanya kinavyopaswa kuwa. Je wewe kuna vitu unafanya haviendani na hili?

Chukua hatua
Upe thamani muda wako ambao umeona unapotea kwa wiki bila ya wewe kukufanyia kazi.
Ondoa masaa kufanya kazi, masaa ya kulala, na masaa ya ambayo utayatumia kwenye safari  na baada ya hapo ugawe muda uliobaki ili uweze kukufanyia mambo hayo matatu hapo juu. 

Endelea kusoma makala za kuelimisha kuyokakwenye blogu hii

Ili upate makala maarumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X