Uongozi ni dhana , taaluma inayompa mhusika
madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale
wanaongozwa naye kuunganisha nguvu , stadi
na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo
yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale
wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi ni dhana, taaluma anayopewa
mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji
kusimamiwa au walioamuliwa kusimamiwa
katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi
ya wote au ya mtu mmoja mmoja.
Soma zaidihapa; Je, Wewe Ni Kiongozi Au Mfuasi?
Hizi hapa ni sifa za kiongozi bora ambzazo anapaswa kuwa nazo
1. KUJIAMINI: Hakuna mfuasi ambaye anapenda kuongozwa na kiongozi ambaye hajiamini na hana ujasiri.
2.UDHIBITI BINAFSI; Mtu ambaye hawezi kujithibiti mwenyewe hawezi kuwathibiti wengine. Kiongozi ajithibiti mwenyewe kwa matendo, maneno na matumizi. Matendo.huongea zaidi ya maneno.
3. HAKI; Kiongozi bora lazima atende haki kwa watu wake wote bila kutumia vigezo vyovyote vya kibaguzi. Iwe ni rangi, jinsi au kabila. Ampe haki anayestahili kupata.
4.MAAMUZI; Kiongozi ambaye hana uhakika juu ya maamuzi yake anaonesha kwamba hana uhakika juu yake mwenyewe. Hawezi kuwaongoza wengine kufikia mafanikio. Kiongozi lazima afanye maamuzi ya muhimu hata kama haungwi mkono na watu wengi.
5. TABIA YA KUFANYA ZAIDI YA ANACHOLIPWA. Hii ndiyo tabia njema ambayo kila kiongozi bora anapaswa kuwa nayo. Wengi sana hujisahau na kutaka kufanya kazi kulingana na kile wanacholipwa tu. Huku wakiwashulutisha wengine kufanya zaidi na wao wakiwatazama tu bila kufanya zaidi. Ben Carson ni mfano mzuri wa kiongozi ambaye aliweza kufanya zaidi ya masaa ya kawaida na kufanya kwa zaidi ya kile anacholipwa.
Soma zaidi hapa; Kama Hawa Wameweza Kwa Nini Wewe Usiweze
6. MALENGO; Kiongozi mzuri lazima awe na malengo yanayopimika. Kiongozi anayekwenda kwa kubahatisha ni kama meli ambayo haina usukani. Muda sio mrefu ataangukia kwenye miamba.
7. UTU UNAOVUTIA; Kiongozi ambaye hajali watu wengine. Anayejali maslahi yake kwanza bila ya kujali maslahi ya watu wengine hawezi kukubaliwa na wafuasi wake.
8. UPOLE NA UELEWA; Kiongozi bora anahitaji kuwa mpole, tayari kuwasikiliza wengine na kutatua matatizo yake.
9. USHIRIKIANO; Kiongozi bora lazima awe mtu wa kushirikiana na watu wengine. Asijifungie ndani bila kujua mambo yanahusiana na watu wake. Kiongozi ni mtu wa watu. Lazima awaulize watu wake wanakumbwa na tatizo gani na atafutevnjia ya kukabiliana nayo.
10. UTAYARI WA KUBEBA MAJUKUMU; Kiongozi lazima awe tayari kubeba majukumu yake. Na asiyaelekeze kwa mtu mwingine ili afanye hivyo. Bali awe tayari kufanya majukumu yake kwa umakini bila hata ya uoga.
Endelea Kusoama makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.
Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA UJAZE FOMU
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante
One response to “Mambo Kumi N (10) Muhimu Kuhusu Kiongozi Bora”
Nimeelewa vinzur sana miiko ya kuw kiongozi Bora