Watu wengi sana wamekuwa wakijiuliza ni muda gani muafaka wanaweza kuanzisha na kukuza biashara?
Hili ni swali ambalo linawatatiza wengi na kwa wengine linaonekana ni kikwazo kikubwa sana cha kuelekea mafanikio. Je, wewe kwako ni kikwazo?
Wapo watu ambao wamekuwa wakijiuliza je waache kazi na kuingia katika biashara au waache kabisa biashara na wasifanye kiujumla? Haya ni makundi mawili ya watu ambayo yote yanahutaji kujibiwa. Jibu la maswali hayo na mengine yatakutwa katika makala hii ya leo.
Soma zaidi hapa; Matendo Hutibu Uoga
Kwa wale ambao wamekuwa wakiamua kuacha kazi na kuamua kuanza biashara wamekuwa wanakutana na changamoto kubwa sana inayowazuia kuelekea mafanikio. Mwanzoni biashara huwa ngumu na hivyo kuwafanya waonekane wamefanya maamuzi mabovu sana
Maisha huwa mangumu zaidi hasa pale mtu anapokuwa na watu wengi sana wanaomtegemea kama familia, wazazi , ndugu jamaa na marafiki. Madeni pia hufanya njia hii kuwa mbovu zaidi
Lakini pia kwa wale ambao wamekuwa wakiamua kuendelea na kazi na kuamua kutofanya kabisa biashara. Hawa nao wanafanya maamuzi mabovu sana
.Watu wa namna hiii wamekuwa wakijifariji kwa kusema kwamba kwa kuwa wapo katika ajira na wana uhakika wa mshahara kila mwezi basi hawahitaji tena kuingia katika biashara,
Pili wamekuwa wakisema kwamba wapo wanakusanya mtaji wa kuanzia biashara na pale mtaji utakapokamilika basi wataanza biashara. Kitu ambacho sio kweli. Kwa maana hakuna siku ambapo mtu anaweza kusema sasa nmepata mtaji wa kutosha kuanzisha biashara.
Sasa nifanyeje?
Zama zimebadilika maisha yamebadilika ajira hatarini na wewe badilika. Tupo katika zama ambapo ajira si za uhakika tena. Tupo katika zama ambapo kazi ambayo zamani iliyokuwa inafanywa na wagu wengi sana sasa inafanya na mashine moja tu. Ajira si za uhakika tena.
Tukirudi kwenye mada kuu ya leo ambapo swali letu linauliza ni “Muda gani Mzuri Wa Kuanzisha Biashara? ” Hili linaweza kuwa ni swali gumu lakini pia wakati huo huo ni swali rahisi sana.
Mimi binafsi nmekuwa siku zote nasisitiza kwamba muda ni sasa, wakati ni sasa, anza sasa. Chukua maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
Kwa yule ambaye tayari yumo katika biashara FANYA YOTE KWA PAMOJA.
Yaani fanya biashara huku ukiwa umeajiriwa. Kwa sababu
1. Utapata sehemu nzuri ya kuanzia.
Kwa sasa upo kwenye ajira. Na mshahara wako unaigia lakini bado upo umuhimu wa wewe kuwa na vyanzo vingi sana vya kukuingizia kipato. Ukianza biashara wakati bado umeajiriwa itakuwa nafasi nzuri ya wewe kuiwezesha na kuikuza biashara yako bila kuitegemea sana. Hii itaifanya biashsra yako iweze kujua kwa kasi. Anza sasa.
2. Fursa nzuri sana ya wewe kupata mkopo.
Ni rahisi sana kwa mtu ambaye ameajiriwa kupata mkopo kuliko mtu ambaye hajaajiriwa.
Kumbe huu ndio muda muafaka wa wewe ambaye upo katika ajira kuanza biashara yako nzuri uipendayo. Badilika sasa, Anza sasa muda ni sasa.
Ili upate makala maarumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA