Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blog ya SONGA MBELE imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuelekea mafanikio. Karibu sana katika makala ya leo
Njia moja ambayo unaweza ambayo unaweza kuitumia chini ya jua na kufanya mtu afanye kitu chochote. Njia ambayo inaweza kukusaidia kushurikiana na wafanyakazi wako vizuri. Njia ambayo itakufanya kushirikianana wanafunzi wenzako vizuri. Njia ambayo itamfanya mtoto mdogo afanye kile unachotaka.
Njia ambayobitawafanya watu unawaooongoza mwende pamoja kwa kufikria na kiutendaji. Njia itakayowafanya wateja wako waendelee kurudi kupata bidhaa zaidi. Je, njia hiyo ni ipi? Ndio ipo njia moja tu. Njia hii ni kumpa mtu kitu ambacho anahitaji
|
Njia moja tu ya kumfanya mtu afanye kike unchotaka |
Kabla sijandelea zaidi ningependa tuone jinsi mvuvi anavyotumia mfano huu kwa kupata kile samaki. Naamini kila mvuvi atakuwa anapendelea kitu fulani.
Nimewahi kumwona mvuvi aliekuwa anapenda pombe sana kiasi kwamba haikupita siku bila ya yeye kunywa pombe . Lakini kila alipoenda kuvua alichukua chombo alijua haswa kwamba alitakiwa kuweka chambo kwenye ndoana na kutupa baharini basi samaki atakuja kula kile chambo naye atakuwa amemnasa samaki.
Umegundua nini rafiki? Japakuwa mvuvi alikuwa anapendelea kunywa pombe lakini alijua kwamba ili ampate samaki lazima ampe kile anachopenda .Je samaki anapenda nini? Samaki anapenda chambo!
Kumbe njia kuu ya kumpata mtu yeyote , kujenga urafiki haraka , kumpata mteja wa kudumu ni kumpa kile anachopenda sio wewe unachopenda.
Mara nyingi sana nimesikia habari za wazazi ambao hukaa na kuwatishia watoto wao kwamba hawapeswi kujihusisha na mapenzi wakiwa wadog ; lakini bado watoto wanafanya hivyo kwa nini? Ni kwasababu hawakupewa au kuambiwa kile walichokuwa wanapenda bali waliambiwa kile wazazi wao walichokuwa wanakitaka .
Wazazi hawakupenda kuona watoto wao wanapata mimba lakini je mtoto alikuwa anapenda hilo?Sasa mtoto anapenda nini? Naamini kila mtoto katika maisha kuna kitu fulani ambacho anapenda kuwa. Ana NDOTOfulani kama mtoto ataelekezwa kwamba kujihusisha kwake na mapenzi kunamfanya asiweze kufikia kitu anachopenda, basi mtoto hataweza kufanya hivyo. Kama anapenda kuwa daktari basi aelezwe kwamba kufanya mapenzi kutamfanya asiweze kufikia udaktari. hicho ndicho mtoto anapenda
Kuna mtoto ambaye alikuwa hapendi kwenda shule , wazazi wake walivyomwambia kwamba anapaswa kwenda shuleni. Basi alikataa kwenda shule ndipo baba yake alipokaa na kujiuliza je mtoto anapenda nini ? basi usiku huohuo baba , mama na kaka zake yule mtoto wakapanga waanze kupaka rangi jiko. Baadae mtoto aliwaona na kutaka kujiunga nao ili aanze kupaka rangi . lakini baba yake alimwambia ili upake jiko rangi lazima uwe umeenda shuleni . baadae wakaenda kulala .Kesho yake aliamka mapema alippofika sebuleni alishangaa kumkuta mtoto ameamka baba alimuuliza “mbona leo umeamka mapema mtoto alimjibu “nataka niwahi shuleni ili na mimi nijifunze kupaka rangi “. Baba alishangaa sana. Kitu gani kilimsukuma mtoto kuamka mapema? Alitaka kwenda shule ili na yeye apate nafasi ya kupaka rangi jiko
Naamini mpaka hapo utakuwa umegundua kwamba njia ya pekee ya kumpata mtu yeyote afanye kile unachofanya ni kumpa kile anachotaka.
Endelea kusoma Makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.
Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea Makala maalumu kutoka songambele. BONYEZA HAPA KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante