Tabia Ya Wanadamu Ambayo Wewe Unapaswa Kuiepuka


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blog ya SONGA MBELE imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuelekea mafanikio. Karibu sana katika makala ya leo.

Kwa kawaida wanadamu huwa tuna mtazamo tofauti kuhusu jambo moja. Wakati katika jambo fulani kuna kundi la watu wanaunaona uzuri katika jambo hilo hilo kuna watu wanauona ubaya. Wakati kuna watu wanataka kwenda kulia wakati huo huo kuna watu wanataka kwenda kushoto. Wakati kuna watu wanafikria chanya katika jambo fulani wakati huo huo kuna watu wanafikria hasi katika jambo hilo hilo.
Wakati wewe kuna kitu kizuri unakiona katika maono yako mazuri ya kuelekea mafanikio wakati huohuo kuna watu ambao wanakuona unapotea. Wakati kuna watu wanataka waone wewe unafanikiwa sana wakati huohuo kuna watu hawapendi kuona unafanikiwa. Wakati kuna watu wanakusuma uweze kufikia mafanikio wakati huo huo kuna wanakuvuta usiweze kuyaelekea mafanikio. Ni uamuzi wako kuamua unaelekea wapi na kwa nini?

Soma zaidi hapa. Ukweli Kuhusu Safari Ya Mafanikio

Kabla sijaendelea zaidi ningependa kukushirikisha hadithi moja nzuri sana ambayo nilihadithiwa na rafiki yangu.
Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa anasafiri huku akiwa na mtoto wake. Wakati safari inaendelea Baba aliamua kupanda farasi peke yake na mtoto akatembea kwa miguu, mara watu wakawaona na kuanza kusema maneno mengi sana.
“Wapo waliosema inakuwaje huyu baba anamtesa mtoto wake kiasi hiki”
Wengine walisema “zipo wapi haki za watoto kama huyu baba anamtesa mtoto wake kiasi hiki”

Baadae baba akaamua kushuka na kumpandisha mtoto wake kwenye farasi na yeye akashuka. Ndipo watu wengine walisema “huyu baba vipi mbona anamdekeza mtoto wake”
“Anamlea mtoto vibaya kiasi kwamba akikua hataweza kujitegemea”

Baada ya hapo baba akaamua kumshusha mtoto wake  na kumwacha farasi atembee bila mzigo wowote ndipo watu wakasema “ ama kweli watu hawajui kuwatumia wanyama vizuri, yaani wanamwacha farasi anaenda bila mzigo na wao wanatembea?”

Baba akaendelea na safari pamoja na mtoto wao na hapo akaamua kumpandisha mtoto wake kwenye farasi lakini pia na yeye akapanda. Watu walipowaona wakaanza kusema “ziko wapi haki za wanyama  mbona hawa watu wanamtesa mnyama”

Kutokana na kipande hicho cha hadithi naamini utakuwa na mengi sana ambayo umejifunza.

Ukweli ni kwamba kitu chochote kitu chochote kike utakachochahagua kufanya lazina watu watakusema maneno mengi sana kuhusu wewe. Usiogope kuchukua hatua na kusongambele. Kalamu itakayoandika historia ya maisha yako unayo wewe mkononi mwako.
Katika kila hatua unayopiga wapo watu watakaokuwa kimya wanasubiri ukosee na wapo watakaokuwa kimya wakikufuatilia kuona utafika wapi na wapo watakokuvuta chini ili uanguke.
Chagua marafiki wako sahihi ili waweze  kukuvijisha pale unapotaka.
Lakini pia chagua vuzuri washauri wako kwenye maisha yako.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasusha kutoka kwenye blogu hii

Ili kupokea makala maarumu kutoka kwenye blogu hii bonyeza hapa ili kujiunga.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


3 responses to “Tabia Ya Wanadamu Ambayo Wewe Unapaswa Kuiepuka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X