Hakuna Kitu Chenye Maana Isipokuwa Tafsiri Binafsi




Habari za leo rafiki yangu na msomaji wa makala kutoka SONGA MBELE BLOG. Matumaini yangu unaendelea vyema na hatua kuelekea mafanikio ndani ya mwaka wetu huu mpya wa 2017. Karibu sana katika makala ya leo, ili tuendelee kujifunza maana hakuna sherehe kwa mwanamafanikio katika kujifunza. Kujifunza kunakufanya unakuwa kijana hata kama una miaka themanini (80) lakini pia kutojifunza kuna kufanya mzee hata kama una miaka ishirini (20). Amua sasa unataka kuwa wapi kwenye kundi la wazee au kundi la vijana. Ila kwa kuwa wewe ushaamua na upo unasoma hapa basi wewe umeamua kuwa kwenye kundi letu la vijana karibu sana.



Hakuna kitu, neno, au tendo lenye maana. Isipokuwa tafsiri binafsi ndizo zinakipa kitu maana.
Mfano ukiwa nyumbani ukamwona mtoto wa miaka miwili akiwa anatembea bila kuvaa nguo utachukulia kawaida sana labda ambacho unaweza kukifanya zaidi ni kutafuta nguo na kumvisha.
Lakini ukiwa pale pale nyumbani umekaa na akapita mtu mwenye miaka 36 akiwa hajavaa kama ambavyo mtoto yule alikuwa hajavaa basi utaanza kusema kwamba huyu mtu katembea uchi au mtu huyu kaweuka. Kwa nini kwa mtoto ionekane kawaida na kwa mtu mzima ionekane tofauti. Ni maana tofauti tunazotoa kwa kitu kilekile.
Kumbe hakuna kitu chenye maana isipokuwa ndiwe unayekipa maana.
Katika mwenelezo wa hili ni kwamba kuna sehemu ya pili ya jambo hili ambayo inasema kwamba
Kitokacho kwa mtu hakiwezi kukudhuru bali kitokacho kwako ndicho chenye uwezo wa kukudhuru
Aongeacho mtu hakiwezi kukudhuru labda uongeacho wewe
Atendacho mtu hakiwezi kukudhuru bali utendacho wewe.
Usikuballi mtu yeyote akuharibie furaha yako kwa namna yako au akuharibie kazi yako kwa namna yeyote iwe ni kwa maneno au matendo maana tumeshaona kwamba anachosema mtu au anachokifanya mtu yeyote hakina maana isipokuwa tu sisi ndio tunakipa maana.

Hakuna kitu chenye maana isipokuwa maana tutakayokipa.
Hakuna neno lenye maana isipokuwa maana tutakayoitoa
Hakuna tendo lenye maana isipokuwa maana tutakayoitoa
Fanya yafuatayo ili uishi vizuri

Angalia unachokiingiza.
Kile ambacho unalisha akili yako kila siku kina mchango mkubwa sana kwenye matendo yako ya kila siku. Akili yako inahitaji kulishwa kila siku kama ambavyo unaililisha tumbo lako kila siku.
Najua  utauliza nitaupaje muda wa kuilisha akili yangu kila siku? Naomba na mimi nikuulize swali je huwa unautoa wapi muda wa kula kila siku?
Sasa unaanza kujiuliza kwamba mbona anahusisha vitu ambavyo havifanani? Hapana sio kwamba havifanani,
Ila kama una uwezo wa kuupata muda wa kula chakula cha kawwaida (kulisha tumbo) basi jua unaweza kuupata na muda wa kuilisha akili yako.
Na katika kuilisha akili yako napendekeza usome vitabu viwe chanzo cha maarifa kwako.

SOMA ZAIDI HAPA; jinsi ya kuepuka kujiua mwenyewe kiakili

Unachokitenda
Unachokitenda kwa asilimia kubwa kinategemea kile unachoingiza, kama utaingiza kitu hasi mara nyingi utakayoyatenda yataendana na kile ulichoingiza, vivyo hivyo kama utaingiza vitu ambavyo ni chanya basi matendo yako yatajaribu kuendana na hicho ulichoingiza. Ndio maana nikaaza kwa kuutaka uingize vitu ambavyo ni chanya ambavyo vitaleta matendo chanya

SOMA ZAIDI HAPA;huu ndio ujumbe aliouandika raisi wa marekani

Matokeo
Matendo huleta mazuri huleta matokeo mazuri lakini pia matendo mabaya huleta matokeo mabaya. Chagua aina ya matendo ambayo ungependa kufanya na anza kuyafanyia kazi sasa.
Nakutakia mwendelezo mzuri wa safari ya kuelekea mafanikio.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


One response to “Hakuna Kitu Chenye Maana Isipokuwa Tafsiri Binafsi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X