Hili ndilo Jambo Muhimu Sana Ambalo Kila Mmoja Analihitaji.


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa songambele blog, imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuelekea na kufikia mafanikio ambayo ni haki yako ya msingi kabisa.

Kwa leo ningependa kuzungumzia jambo moja ambalo kila mmoja wetu analihitaji katika maisha yake ya kila siku ili aweze kuendelea na kufikia mafanikio makubwa sana. Jambo lenyewe ni lipi?
Jambo lenyewe ni MAARIFA.

Kuna aina mbili za maarifa ambazo ni maarifa ya kiujumla na maarifa ya kitaalamu.

1. Maarifa ya kiujumla.
Maarifa ya kiujumla ni elimu ambayo inatolewa kwa upana wake katika sehemu nyingi sana. Ni maarifa ambayo yanatolewa hata vyuoni, na kwa bahati mbaya vyuo havijajikita kuona ni kwa namna gani maarifa hayo mtu anaweza kuyatumia kupata mafanikio

Soma zaidi hapa; Utavuna ulichopanda

Mafanikio ni huduma

Maarifa yenyewe tu hayawezi kuvuta pesa mpaka pale yatakapokuwa yamepangiliwa na na kuwekewa mipango. Lakini mipango peke yake haitoshi mpaka pale itakapoanziwa kufanyiwa kazi.

Kutolielewa jambo hili ni hatari sana maana watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba elimu ni ufunguo wa maisha. Hakuna kitu kama hiki. Elimu itakuwa ufunguo wa maisha pale itakapowekewa mipango na kuanza kufanyiwa kazi.

Soma zaidi hapa;  Jinsi ya Kuweka  Usawa Katika Mapato Na Matumizi

Watu wengi wamekuwa wanachanganya na kutoa maana tofauti kuhusu mtu mwenye elimu na maarifa. Wamekuwa wanasisitiza kwamba mtu mwenye elimu lazima awe ameenda shuleni au chuoni na kupata elimu kutoka katika taasisi za elimu. Jambo hili sio kweli.

Njia za kupata maarifa.
Hakuna mtu ambaye anajua kila kitu. Kila mtu kuna kitu ambacho atakuwa mtaalamu na atakifanya vizuri huku mwenzake akifanya vizuri juu ya kitu kingine.

Vyanzo vya maarifa vipo vingi sana kutegemea na aina ya maarifa ambayo mtu anahiitaji kwa hiyo kitu cha kwanza ambacho mtu anahitaji kujua ni kuchagua aina gani ya maarifa unataka kupata. Ukishachagua aina gani ya maarifa unahitaji basi hapo utachagua jinsi ya kuyapata maarifa ambayo yanapatikana kwenye vyanzo vilivyowekwa hapo chini.

Maarifa ya kitaalamu.
Hii ni elimu ambayo kila mtu anaweza kuipata tena bila gharama au kwa gharama ya chini sana. Kama kawaida kabla ya kupata elimu hii inakupasa ujiulize ni kwa nini unataka kupata elimu hiyo na itakusaidia nini katika kile ambacho unataka kufanya. Baada ya hapo unaweza kuamua ni kwa njia gani unaweza kupata maarifa hayo.

Vyanzo vya maarifa vinavyofahamika ni
1. Ujuzi binafsi.
2. Ujuzi kutoka kwa wengine..
3. Mashuleni na vyuoni
4. Kutoka kwenye maktaba (hapa kwenye suala la maktaba ni muhimu sana kutambua kwamba katika zama za sasa mtu unaweza kutembea na maktaba yako  popote ulipo iwe ni kwenye simu au kompyuta yako).
5. Kupitia semina, webna na matamasha mbalimabali

Igundulike kwamba maarifa ni kitu ambacho binadamu anakihitaji kila siku ili kuweza kufika sehemu anapotaka.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika makala ya leo.

Maarifa bila kuyafanyia kazi basi hayana maana. Maarifa sharti yawekewe mipango itakayofuatiwa na utekelezaji.

Usipochagua aina ya maarifa ambayo unataka kupata utajikuta ukiingiza kila kitu, maarifa yanayokufaa na yasiyokufaa. Ni sawa na kuingia maktaba na kuanza kusoma kila kitabu unachokiona mbele yako. Hapa utasoma vitabu vingi sana ambavyo vinakufaa na ambavyo havikufai. Chagua ni maarifa gani unahitaji sasa na anza kuyatafuta.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
AsanteBONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X