Kama Sio Wewe Ni Nani, Kama Sasa Ni Lini?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za SONGAMBELE BLOG. Karibu sana katika makala ya leo.

Watu wengi tumezaliwa na VIPAJI mbalimbali ambavyo kama tutavifanyia kazi basi tutapiga hatua kubwa na kufikia mafanikio. Ukomo wa kutumia kipaji chako unajiwekea mwenyewe, hakuna wa kukuwekea kikomo katika matumizi ya kipaji chako.

Maisha yako sio tu kuhusu wewe. Bali maisha yako ni juu au jinsi gani unaongeza thamani kwa watu wengine.

Hii ni habari mpya ambayo binafsi sikupenda kuitoa kwako nikiwa wa kwanza lakini nimelazimika kufanya hivyo.

Kama utakua umejawa na umimi au ubinafsi basi naweza kusema sahau kuhusu mafanikio.

Mafanikio yanatokea pale unapotoa huduma kwa watu. Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema “lengo la maisha yetu ni ni kuongeza  thamani kwenye maisha ya watu wengine na wale wanaofuata” (vizazi vinavyofuata)

Sasa tunaongezaje thamani kwa watu wengine?

Soma zaidi hapa; Mbinu za kukusaidia kufikia ndoto yako kabla mwaka haujaisha

Tunaongeza thamani kwenye maisha ya watu wengine tunapokuwa wajasiriamali. MJASIRIAMALI ni nani?

Mjasiriamali ni mtu anayetatua matatizo ya watu. Basi hakuna kitu cha zaidi ya kutatua matatizo ya watu. Nani anatatua matatizo ya watu na anatumia nini?

Hapo ndipo tunarudi kwenye kichwa cha makala yetu na kusema kama sio wewe ni nani? Kama sio sasa ni lini?

Sasa nakuuliza swali jinguine? Unapenda kutatua matatizo ya watu wangapi?

Kumi, mia moja, elfu moja laki au millioni na zaidi.

Najua utakua na namba ambayo utakua umechagua. Namba ya watu ambayo utakua umechagua  ndiyo itakuambia kiasi cha mafanikio unachotaka kufikia. Ukichagua namba ndogo maana yake unataka mafanikio kidogo, ukichagua namba kubwa maana yake unataka mafanikio mkubwa.

Usifanye kosa hata kidogo, kumbuka kila mtu duniani kuna kitu anafikiria kufanya kumbe wewe amua sasa kufanya, anza kufanya na fanya kwa ubora zaidi na toa thamani kubwa sana.

Soma zaidi hapa; Hili ni kosa ambalo watumiaji wengi wa mtandao hufanya

Kazi ya kufanya leo:

  1. Andika chini kile ambacho imani ni kipaji chako. Hivi ni vitu ambavyo uwa unavifanya vizuri. Andika ni wapi unaweza kutumia hivi vipaji hasa kwenye maisha yako.

     SOMA ZAIDI HAPA; Kipaji ni nini?

Jewajua unauwezo sawa na hawa?

  1. Angalia na andika ni kwa namna gani unaweza kutatua matatizo ya watu. Andika walau mbimu tatu.
  2. Chagua moj ya kuanza nayo ili kuanza kunboresha maisha ya watu.
  3. Anza sasa

    Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

    Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
    Ni mimi rafiki na ndugu yako
    Godius Rweyongeza
    Tuwasiliane
    godiusrweyongeza1@gmail.com


2 responses to “Kama Sio Wewe Ni Nani, Kama Sasa Ni Lini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X