Kama Unapanga Kufanya Jambo Rahisi Maisha Yako Yatakuwa Magumu Kama Unapanga Kufanya Jambo Gumu Maisha Yako Yatakuwa RahisiHabari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako penswa ya songa   mbele karibu sana katika Makala ya leo ambapo tunaenda kujfunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu.
Kujjifunza ni kitu ambacho hatupaswi kuschoka kufanya kila siku na tunapasa tufanye hivi maisha yetu yote, hujaishi leo kama hujajifunza kitu kipya leo.
Mara nyingi ukimwambia mtu kufanya kitu kipya atakwambia kwamba hakijawahi kufanyika au watu watanionaje au ataanza kukwambia kwamba watu fulani walifanya kitu hicho.
Hivi mambo tunayoyatumia leo  kama watu wangeacha kufanya hapo mwanzo kwa kuweka visingizio kwama watu wataowaonaje leo vingekuwepo? Tazama vitu vilivyokuzunguka vyote vimetokana na watu waliothubutu na kuanza kufanya, tazama nyumba ulimokaa sasa hivi ilitokana na watu waliochukua hatua na kuamua kuleta mabadiliko. Nyumba hazikuwepo kwenye uumbaji wa dunia lakini kutokana na watu kuthubutu kwa watu basii wu waliweza kubuni na kujenga nyumba. Watu hawa hawakuhofu ni kwa watafikiriwaje na watu wengine bali waliweza kuchukua hatua. Chukua hatua sasa!!
Tazama gari ambalo huwa unafurahia linakusafirisha, tazama nguo ambazo umevaa, hivyo tu ni baadhi ya vitu ambavyo vimetngenezwa na watu waliothubutu. Thubutu sasa!!
Je chanzo cha mambo haya yote haya ni nini?
Uoga.                      
Ndio uoga . uoga unaua mambo  mengi  ya muhimu sana ambayo watu wanapaswa kufanya kwa ajili ya maendeleo. Sipati picha kama  mti, ungekuwa na uoga basi mti wa mita kumi ungekua kwa mita moja tu. Ni ajabu sana kuona kiumbe ambacho hakina akili na utashi hakiogopi lakini bindamu mwenye akili anaogopa!
Wanasayansi wamegundua kwamba binadamu anatumia akili yake kwa kiwango amacho kipo chini ya asilimia kumi {10%}. Hee maajabu!
Hivi kama mpaka sasa unatumia akili y ako kwa asilimia saba 7% na ukaongeza mara mbili Zaidi yake utafanya mambo kiasi gani? Yaani utakuwa una uwezo wa kufanya mambo makubwa sana.  Sasa kitu gani kinakuzuia rafiki? Jibu ni uoga!
Kuridhika
Kitu kingine kinachowazuia watu kufanya kazi na kufikia mambo makubwa ni kuridhika.  Wakati naandik Makala hii kuna mtu alinipiga simu na wakati tunaongea akawa ananiambia kwamba maisha ni magumu hkuns mvua , akazidi kuniambia kwmba hali itakuwa mbaya kufikia mwezi wa tisa basi hali itakuwa mbaya kutokana na uhaba wa chakula
Nikamuuliza sas utafanyaje kama hali itaendelea hivi; akaniambia sasa utafanyaje maana hali imekuwa hivi kwa miaka kadhaa hakuna jisdi ya kufanya labda mpaka pale serikali itakapobadili hali hiyo.
Nikamwambia kwamba binadamu tumeubwa kwa akilli yenye uwezo mkubwa sana  ambayo kama tuaitumia vizuri sana akili tunaweza kufanya mambo makubwa sana hata ambayo haya hayajawawhi kufanyika katika sayari hii ya tatu.
Nikazidi kumwambia kwamba sikuzote llikitokea tatizo jiulize ni kwa namn gani naweza kulitatua tatizo hili?
………………………………………………………………………………………………
Kuna mambo mengi sana tuliongea lakini kun kauli moja aliongea ambayo ilinifurahisha aliposema “afadhali niendelee kufanya mambo rahisi mambo yangu yatakuwa rahisi kuliko kufanya mambo magumu maisha yangu yakawa magumu”
Nilimjibu hivi;
Kama unapanga kufanya kitu rahisi maisha yako yatakuwa magumu na kama unapanga kufanya kitu kigumu maisha yako yatakuwa rahisi.
Rafiki wangu alianza kwa kusema maisha ni magumu lakini bado antaka kuendelea kufanya vilevile kwa mazoea. Anaona kuendelea kufanya hivyo hivyo kwa mzazoea utakuwa mtelemko.
Maneno yanaonesha hataki kitu Fulani lakini matendo yanaonesha amwridhika
Ulishawahi kuwahi kujiuliza siku ya kwanza ulipoanza jufanya kituu kipya ulijisikiaje. Bila shaka hukujisikia vizuri lakini baadaya kufanya mara kwa mara basi ukajikuta unaweza kufanya vizuri tena vizuri Zaidi. Mazoea hujenga tabia.
Chukulia maisha kama kama kitu ambacho kinapimwa kwenye kipomo cha moja mpaka kumi, na wewe upo kwenye kipimo cha tano. Kutoka tano mpaka kumi, utajumuisha kutoridhika, lakini baada ya muda utaanza kujisikia vizuri. Hii ni baada ya kuanza kufanya na kufanya bila uoga, utajikuta umeweza kufikia hatua ya kumi. Inawezekana.
Mambo ya kufanya leo
1.       Angalliani hatua gani unataka kufikia kimafanikio
2.       Weka mipango ya kufika huko
3.       Angalia ni vikwazo gani unawezea kukutana navyo wakati wa kuelekea unapotaka kufikia
4.       Anza kuondoa vikwazo ambavyo vitakuzuia kufika unapotaka. Njia ya kuondoa vikwazo hivi ni kuanza.
5.       Anza kupambana na changamoto ndogo ambazo zinajitokeza.
Anza sasa
Muda ni sasa
Badilika sasa
Songa mbele sasa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X