Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu
Mara nyingi likitokea kosa lolote mtu atamtafuta mtu wa kulalamikia.
Hivi ulishawahi kugundua kwamba ukimunyooshea mtu kidole kimoja vitatu vinakuelekea wewe na kimoja kitaelekea juu kama ishara ya ushahidi.
Hii ni kuonesha kwamba wewe ndiwe unayechangia asilimia 75℅ ya makosa yako na changamoto zako zinazojitokeza, na mwingine unayemunyooshea kidole anachangia asilimia 25% ya makosa. Kumbe hata kama angetimiza wajibu wake bado kosa au kikwazo hicho kingetokea kwa sababu wewe kama mhusika unachangia asilimia 75 ya makosa yote.
Je unahitaji mabadiliko wewe kama wewe?
Je mnahitaji mabadiliko kama kikundi?
Sasa ni muda wa kuacha kuwa na matamanio na kuanza kufanya.
Soma zaidi hapa; Je, wewe una matamanio au ndoto?
Kitu kizuri kitakachokufanya ufike unapotaka ni nidhamu juu ya kile unachofanya
Nidhamu ni mtaji nambari moja ambao unapawa kulipa kwa ajili ya mabadiliko na matukio mazuri ya baadae.
George Washnton anasema
Nidhamu ni roho ya jeshi na hulifanya jeshi kushinda au kushindwa
Nidhamu ni njia ya kuelekea mafanikio
Nidhamu ni njia ya kukuletea mabadiliko
Nidhamu ni kukubali kwamba wewe ni mhusika mkuu kwa kila kitu maishani mwako.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA