Kama Utashindwa Ni Juu Yako Na Kama utashinda Ni juu yako


 Habari za leo rafiki yangu na msomaji wa makala kutoka SONGA MBELE BLOG. Matumaini yangu unaendelea vyema na hatua kuelekea mafanikio ndani ya mwaka wetu huu mpya wa 2017. Karibu sana katika makala ya leo, ili tuendelee kujifunza maana hakuna sherehe kwa mwanamafanikio katika kujifunza. Kujifunza kunakufanya unakuwa kijana hata kama una miaka themanini (80) lakini pia kutojifunza kuna kufanya mzee hata kama una miaka ishirini (20). Amua sasa unataka kuwa wapi kwenye kundi la wazee au kundi la vijana. Ila kwa kuwa wewe ushaamua na upo unasoma hapa basi wewe umeamua kuwa kwenye kundi letu la vijana karibu sana.

Mara nyingi likitokea tatizo huwa unakimbia kumtafuta mtu yeyotwe wa kulalamikia, na huyu huwezi kumkosa maana hapa wapo wat wengi ambao wamekuzunguka ambao unaweza kuwatupia mpira lakini wewe ndiye mtu muhimu sana katika maisha yako ambaye anachangia kwa asilimia kubwa sana katika mafanikio yako  au kushindwa kwako.
Hivi ulishawahi kugundua kwamba ukimunyooshea mtu kidole kimoja basi vidole vitatu hukuelekea wewe? Na kidole kimoja huelekea juu kama ishara ya ushahidi kwa Mungu?
Soma zaidi hapa: kupe hawa wananyonya muda wako kila siku
Hii ni kuonyesha kwamba wewe ndiwe unayechangia asilimia sabini na tano [75%] huku wenzako wakichangia aslimia ishirini na tano [25%].
Hii inaonesha kwamba hata kama wenzako wangetimiza majukumu yao kwa asilimia mia moja bado ungeshindwa kufikia kile ambacho umanga kwa sabau wewe ndiwe unayechangia asilimia kubwa sana kwenye matokeo yako. TIMIZA SABINI NA TANO ZAKO KWANZA.
Je unahitaji mabadiliko wewe kama wewe?
Je,  mnahitaji mabadiliko kama kikundi? Sasa ni muda wa kuacha kuwa na matamanio na kuanza kufanya
Soma Zaidi hapa;  je wewe una matamanio au ndoto?
Kitu kizuri kitakachokufanya ufike unapptak  ni nidhamu ya kile unachofanya. Nidhamu ni mtaji ambao unaulipa kwa ajili ya mabadiliko.
Nidhmu ni kufanya kile ambacho unapaswa kufanya kwa ajili ya matokeo ya mazuri ya baadae
Washington aliwahi kusema “nidhamu ni roho ya jeshi ambayo inalifanya jeshi dogo kuwa na ushindi wa haki ya juu”
Nidhamu ni njia ya kuelekea mafanikio
Nidhamu ndiyo huleta utofauti
Ndiyo huleta mabadiliko
Nidhamu ndiyo hukufanya kukubali kwamba wewe ndiwe mhusika mkuu kwa kila unachofanya
Kama unataka kubadilidha dunia jibadilidhe wewe kwanza na mabadiliko mengine yatafuata

Godius Rweyongeza





Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X