Kama Watu Wote Watakuwa Matajiri Maskini Watatoka Wapi?



Kuna baadhi ya watu wamekuwa na imani kwamba haiwezekani watu wote kuwa matajiri. Wengine wanasema kwamba haiwezekani watu wote kuwa matajiri na wengine wansema haiwekani mtu kuwa tajiri lakini bado akaendelea kumwabdu Mungu.
Huu ni mtazamo hasi ambao watu wanao ambao hauwezi kukufanya usonge mbele. Siku zote watu wenye mtazamo huu huwa napenda kuwaambia wasome shairi hil kwa umakinii.

Kama unafikiria umepigwa,umepigwa
Kama unafikiri umeshindwa,umeshindwa
Kama unafikiri huwezi,huwezi
Kama unataka kushinda lakini unafikiri huwezi,karbia huwezi.

Kama unafikiri utapoteza,umepotea
Kwa sababu katika dunia ushindi unaanza na msukumo wa ndani ya mtu,
Hiyo inaitwa hali ya akili.(state of mind).

Kama unafikiri umepitwa na wakati,umepitwa
Inabidi ufikiri mbali kujiinua
Inabdi ujiamini mwenyewe kabla ya kushinda tuzo.

Vita vya maisha hashindi mtu mweye nguvu au mwenye mbio za haraka
Vita vya maisha anashinda mtu ANAYEFIKIRI ANAWEZA.

Watu ambao wamekuwa wakifiri haiwezekani kwa watu wote kuwa matajiri wamekuwa wakiuliza maswali kama  “kama kila mtu atakuwa na kila kitu nani atanunua kwa mwenzake?
Wamekuwa wakiendelea kujifariji kwamba lazima wawepo matajiri na maskini ili kuwepo na mlinganyo sahihi. Sio kweli.
Kwa kuwa tunajua moja ya  lengo kuu la binadamu kuwepo duniani ni kuitawala dunia, na hatuwezi  kuitawala dunia dunia wakati tukiwa tunaamini kwamba haiwezekani sisi kufanya kitu na kufanikiwa. Dunia hii inatawaliwa na watu wenye tabia na sifa za kiuongozi.
Soma zaidi hapa; je wewe ni kiongozii au mfuasi.
Kufikria hasi sio tabia ya kiongozi ambayetaka kuitawala dunia
Pili  sio kwamba bidhaa zitakosa wanunuzi  kama watu wote watajihusisha na biashara. Chukuli a mpo watu wane ambapo kila mtu ana bidhaa yake kama inavyoonekana hapo chini
A anauza nguo
B  anaauza viatu
C anauza  vitabu
D  anauza simu
Kama kilakitu kinauzwa kwa  Tsh 15000
Yeyote atakayetaka kununua nguo lazima ataenda kwa A, na watu watatu wote wakichukua nguo ina maana A atatengeneza  tsh 45,000  vivyo hivyo  kwa mtu atakayehitaji  viatu atamwndea  B. na kama watu wote waliobaki watanunua viatu. Basi mtu B atatengeza tsh 45,000.Kitu kama hicho tuna tegmea kitokee tena kwa mtu C, na D. amabao pia tutetgemee watengeneza  tsh 45,000 kila mmoja.
Tatu fahamu kwamba  pesa huwa haiishi na unaweza  Kuitumia noti hiyohiyo  miaka nenda miaka rudi.
Kadri unavyokuwa na pesa ndivyo unavyoweza kuongeza pesa zaidi  kwenye mzunguko, na hivyo watu wengine kufaidika zaidi.
Utaingiza nini kwenye mzunguko kamz hauna pesa?
Pesa itaonesha tabia yako halisi,
Kama ulikuwa mchoyo ukiiiipata pesa utaendelea kuwa mchoyo na kama ulikuwa mcha Mungu ukipata pesa utaendelea kuwa mcha  Mungu. Kama unawasaidia msakini utaendelea kuwasasidia maskini,  na tabia zako nyingine  zitabaki kama zilivyo mpaka  utakapo kuwa umebadilika wewe.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X