Mara nyingi huwa watu wanaamini kwamba mtu unapaswa kuishi maisha kiasi kwamba ukifa utokee kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti .
Lakini je hii ni kweli? Shida sio kutokea mbele ya gazeti lakini je ulipotokea mbele ya gazeti, gazeti lenyewe limeandika nini juu yako.Kuna watu wametokea mara nyingi sana mbele ya magazeti wakiwa wameandikwa maneno tofauti. Chukulia mtu katokea mbele ya gazeti na gazeti kenyewe limeandika,
MUUZA MADWA YA KULEVYA AFARIKI DUNIA au
JAMBAZI AUAWA NA POLISI DAR.
Je kwa hali hii kuna haja ya kuishi maisha kiasi kwamba ukifa utokee mbele ya gazeti?
Simaanishi kwamba kutokea mbele ya gazeti ni kitu kubaya kwa sababu wapo watu wengi sana wametokea mbele ya magazeti wakiwa wamefanya mambomazuri sana, siwezi kuwataja wote katika makala hii maana ni wengi sana, ila kitu cha msingi ninachopenda kusisitiza ni kwamba tuishi maisha kama alivyoyataja Aldous Huxley kwenye kitanda chake alipokuwa anakarbia kufariki alisema
“Tuwe wakalimu kwa kila mtu”
Maisha mazuri ni yale ambayo unaishi kwa adabu na ukarimu. Unaishi vizuri kwa kila mtu, na kila sehemu unapokutana na mtu.
Kiukweli kama utaishi maisha ya kuwafanya watu wenye furaha hata kama utamfanya mtu mmoja mwenye furaha kwa siku basi utakuwa unastahili tuzo.
Robert sharma anasema
“ulipozaliwa ulilia wakati dunia wakati dunia ilishangilia, ishi maisha kiasi kwamba ukifa watu walie wakati wewe ukishangilia”
Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA