Lifahamu Kusudi Lako


Habari za leo rafiki yangu na msomaji wa makala kutoka SONGA MBELE BLOG. Matumaini yangu unaendelea vyema na hatua kuelekea mafanikio ndani ya mwaka wetu huu mpya wa 2017. Karibu sana katika makala ya leo, ili tuendelee kujifunza maana hakuna sherehe kwa mwanamafanikio katika kujifunza. Kujifunza kunakufanya unakuwa kijana hata kama una miaka themanini (80) lakini pia kutojifunza kuna kufanya mzee hata kama una miaka ishirini (20). Amua sasa unataka kuwa wapi kwenye kundi la wazee au kundi la vijana. Ila kwa kuwa wewe ushaamua na upo unasoma hapa basi wewe umeamua kuwa kwenye kundi letu la vijana karibu sana.

Soma zaidi hapa ; Huu ni utumwa ambao kila mtu anapaswa kuuepuka 

Lifahamu kusudi lako

Mwanadamu sio mtu ambaye ametokea tu kwa bahati mbaya, ni mtu ambaye yupo kwa sababu kubwa kwa sababu fulani. Aliyetuweka duniani MUNGU ndiye aliyetutengeneza na sisi ni bidhaa zake.

Kusudi la kutengeneza huwa linafahamiwa na mtengenezaji wake.
Kwa mfano;
Matumuzi ya kalamu ni kwa ajili ya kuandika ni kazi ambayo ilifikiriwa na mtengenezaji, wake.  Matumizi ya kalamu sio kukata au kulia chakula.
Hata kama kalamu itauzwa bei mara kumi zaidi ya kisu lakini haitakuja kutokea kwamba kalamu imefanya kazi ya kukata. Kama utaitumia kwa shughuli yeyote ile tofauti na ile ambayo ilikusudiwa na mtengenezaji basi utakuwa umeitumia visivyo.
Vivyo hivyo binadamu amezaliwa kwa kusudi fulani ambalo ni maalumu ambalo anapaswa kulifanya.  Ukigundua ambacho unapaswa kufanya hapa duniani ni kugundua kusudi lako.
Na ukigundua unachopaswa kufanya basi kinakufanya  kuwa WEWE.

Ili kujua kazi ya kitu fulani lazima umuulize aluyekitengeneza na kujua kazi au kusudi lake la kuengeneza hicho kitu.
Kugundua kusudi lako ni kugundua eneo ambapo unapaswa kutoa huduma.

“Usipende kuwa mtu wa kutumia unaweza kuishia kutumiwa

Godius Rweyongeza 

Usiishi maisha kwa kufanya kila kitu na kwenda kila sehemu. Je umewahi kusikia kwamba vyuoni kuna maprofesa wa sheria, historia, biologia, kemia? Je, wapo?
Kama lengo ni kila sehemu utapoteza, na hutafika unapotaka.
Chagua vitu vichache vya kufanya na vifanye tena kwa ubora zaidi.

Jinsi ya kugundua kusudi lako

  1. Vipaji vilivyo ndani yako?
Kuna vipaji ambavyo vimo ndani yako, kuna dhahabu ndani yako imelala, ambayo unaweza kuitumia vizuri sana kukufanya ufikie mafanikio makubwa sana.
Soma zaidi hapa; vipaji ni nini
2. Ufunuo
Haya ni maono ya kiroho ambayo mtu anayapata. Mara nyingi ufunuo hutoka kwa Mungu. 
Kufahamu vizuri kuhusu ufunuo unaweza kuongea na viongozi wako wa kiroho wanaweza kukuelelekeza vizuri zaidi.
Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X