Ushindi Sio Mwisho, Ushindi Ni Mwanzo


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala kutoka SONGAMBELE BLOG, karibu katika makala ya leo.

Kila mtu atafutaye mafanikio hupenda kufikia mafanikio. Kila mwanadamu angependa kuona anashinda na kupiga hatua na kufikia hatua nzuri. Mafanikio kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni ushindi. Ushindi ni mjumuiko wa siku nyingi za ushindi.

Mara nyingi ushindi ambao huwa tunauona huwa unaonekana kama umetokea  kwa siku hiyo lakini huwa ni mjumuiko wa siku nyingi sana za ushindi.

Timu ya mpira wa miguu inaposhinda kwenye mchezo sio tu kwamba mazuri yametokea siku hiyohiyo ya mechi bali ni matokeo ya maandalizi mazuri ya kila siku uwanjani. Kumbe ni matokeo ya ushindi wa kila siku kwenye mazoezi.

Ni kwa mantiki kama hiyo msanii anapofanya vizuri kwenye jukwaa au anapotoa wimbo mzuri bado ni matokeo ya siku moja ambayo aliitumia vizuri kwenye maandalizi. Kumbe kuna umuhimu mkubwa sana  wa kuitumia vizuri leo, ili leo iwe mchango mzuri sna kwenye matokeo yako (ushindi wako). 

Soma zaidi hapa;   Ijue siku rafiki kwako

Sasa baada ya ushindi kitu gani kinafuata?

Kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia huwezi kufunga goli la pili wakati bado unashangalia goli la kwanza.

Kama ambavyo ushindi ulitangulia  na maandalizi, vivyo hivyo baada ya ushindi maandalizi ya ushindi wa pili yanfuata.

Kumbe siku zote usitumie muda mwingi sana kushangilia jambo ambalo umelifanya bora zaidi. Shangalia ushindi na uendelee kujiandaa tena kwa ajili ya mashambulizi yanayofuata.

Huwezi kufunga goli la pili wakati bado unashangalia goli la kwanza na ushindi sio mwisho bali ushindi ni mwanzo.

Hata ukiangalia mifano niliyotoa hapo juu, mifano ya timu na msanii katoa wimbo mzuri,bali baada ya hapo timu inajiandaa kwa ajili ya mechi inayofuata na msanii anaanza kujiandaa kutoa wimbo unaofuata. Hapo ndiyo tunaelewa na kusema kwa pamoja kwamba

“Ushindi sio mwisho, ushindi ni mwanzo”

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X