Vipaumbele vyako ni vipi?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu
 Katika maisha tuna mambo mengi sana ya kufanya. Yote kwa pamoja ni mambo yanyotuelekezaa kwenye mafanikio. Ila ingawa yote ni muhimu yanatofautiana kwa vipaumbele. Mambo yote haya hayawezi kuwa na vipaumbele sawa. Kumbe kama unataka kufanya mambo manne ambayo ni A,B,C,D basi unahitaji uyapangalie vizuri sana. Jua kipi kinapaswa kuanza na kipi kinafuata.

Je, kinachoanza kinaongeza thamani gani kwako?

Kumbe kama una mambo A, B, C, D yape namba kadri ya kipaumbele chako, 

mfano

       A-Ni namba 1

C- Ni namba 2

D- Ni namba 3 na


B-Ni namba 4

Anza kufanya kipaumbele namba moja; ukimaliza kipaumbele nambari moja, fanya kipaumbele nambari mbili na kuendelea mpaka mwisho.

Hilo suala sio kwa vipaumbele ndani ya siku husika bali hata vipaumbele vyako vya wiki, mwezi na hata mwaka mzima.

Ukiamka inashauriwa uandike kwanza mambo ambayo ungependa kufanya ndani ya siku husika.

Inashauriwa uandike mambo sita (6) ya kufanya ndani ya siku husika na yapangilie kadri ya vipaumbele vyako.

Nakushauri wakati unaangalia vipaumbele vyako na kuvipa namba, viwekee na muda ambao utafanya kazi ndani ya kipaumbele husika.

Jitahidi ukifanya kipaumbele husika ndani ya muda uliopanga kukifanya.

Utumie muda wako vizuri maana kama kuna jambo labda umelipa muda mrefu mwanzoni unaweza kuanza taratibu ukijifariji kwamba unao muda wa kutosha na hivyo ukakaribia mwishoni na kugundua muda hautoshi.

JAMBO
NAMBA YA KIPAUMBELE
MUDA
A
1
Masaa 3
B
4
Saa 1
C
2
Masaa 2:30
D
3
Dakika 45

Wakati unaanza kufanya jambo A utaona muda upo wa kutosha hivyo kuanza kufanya kwa utaratibu mkubwa sana.

Lakini baadae utagundua muda umepungua na hautoshi na kuanza kukimbizana na muda.

Jambo hili linaweza kupelekea kutofanya vizuri kazi yako au kutoikamilisha, kutoipa thamani inayo stahili.

Kumbuka muda ni rasilimali. Ambayo hatuwezi kuipata sehemu yoyote ile kwa kuinunua. Hivyo siku zote itumie kila sekunde vizuri. Anza kwa kujiuliza kipaumbele chanko ni kipi. Vipaumbele hutofautiana katika masomo, katika ibada, marafiki.

Naomba nikuulize tena vipaumbele vyako ni vipi?

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X