Hili Hapa Jambo La kuogopa


Muda  ambao mtu anaupoteza akiwa na hasira,
Nguvu ambayo mtu anaipoteza akiwa na hasira, kupiga majungu na kuwachukia watu unatosha sana kumfanya kuwa tajiri katika maisha yake yote.

Nwanadamu anapoteza robo tatu ya maisha yake yote bila kufanya kitu.
Napolleon Hill
Katika maisha yangu sijawahi kusikia kwamba mtu kafaidika kutokana na hasira. Sijawahi kusikia kwamba hasira imezalisha kitu kilichobora ambacho mwanadamu ananufaika, sijawahi kusikia kwamba hasira ilimzalisha mwanafalsafa bora.

Hasira itakufanya upoteze muda wako mkubwa sana

Pombe na sigara hazina madhara makubwa sana kama yalivyo madhara ya hasira.

Kumbe kumchukia mtu hakuna faida kwetu badala yake kuna hasara kubwa sana kwenye maisha yetu.

Njia nzuri ambayo unaweza kuitumia katika kuhakikisha unaepukana na hasira ni kulipa wema kwa ubaya. Achana na vitu ambavyo vinasema jino kwa jino maana ni kauli ambayo itakufanya ubaki na hasira muda wote hivyo kukufanya uendelee kurudi nyuma kwa kufikiria vitu ambavyo huvihitaji wakati unapohitajika kuwa mahara fulani.

Tambua kwamba kiwango cha mafanikio kinapimwa kwa idadi ya watu unaowahudumia na sio watu unaowachukia. Kiwango cha mafanikio kinapimwa kwa idadi ya watu waliokuzunguka ( watu uliowavutia kwako) na sio watu  uliowatenganisha.

Njia nyingine ya kuepukana na hasira ni kuepuka mabishano na watu, epuka sana mabishano maana hayana tija kwako. Mabishano yatakufanya upoteze nguvu kubwa sana kuongea, lakini sio tu kwamba utapoteza nguvu bali utapoteza na muda mwingi katika kubishana na  mtu ambaye pengine ni vigumu kumbadilisha.

Kama unataka kumbadilisha mtu usisubiri umbadirishe ukiwa na hasira, hutaweza, mbadilishe ukiwa  hauna hasira. Na njia nzuri ya kumbadilisha mtu yeyote ni kuanza kujibadilisha wewe mwenyewe.
Jibadilishe katka utendaji wako. Jibadilishe katika uongeaji wako, na jibadilushe katika tabia zako wengine watafuata. Huwezi kuibadili dunia bila kujibadili mwenyewe.

Soma zaidi hapa Njia Ya Kutmia Kumfanya Mtu Afanye Unachotaka Afanye

Kukaa na hasira ni sawa na kuendelea kushikilia kaa la moto ukiwa na lengo la kumrushia mtu kaa hili la moto. Ni wewe utauungua tu.

Buddha

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X