Habari za leo na ndugu msomaji wa blogu ya songa mbele karibu sana katika makala ya leo ili tupate kujifunza kitu kipya cha kutufanya tusonge mbele
Mara nyingi watu wanachanganya kati ya kupenda na kupata kitu.
Kupenda kitu ni tofauti sana na kupata. Mfano mtu akisema napenda kupata gari ni tofauti kabisa na kupata gari
Kukipenda kitu ni kukitamani tu kitu bila ya kuweka juhudi ya kuhakikisha umekifikia hicho kitu.
Kupata kitu kunakuhitaji uweke juhudi na nguvu na kufuata kanuni fulani ambazo zitakukufanya uweze kufikia hatua fulani ya mafanikio.
Kupenda ni hatua moja ambayo inakupelekea kupata.
Kama unapenda kupata maembe hutaishia tu kusema napenda maembe bali utaweka juhudi za kupanda mti kuumwagilia, kuweka mbolea, kuhakikisha umekua na kufikia hatua nzuri na baadae ndipo utakuja kuvuna na kupata matunda.
Soma zaidi hapa; Je, Wewe Una Matamanio Au Ndoto?
Utavuna Ulichopanda
Kumbe rafiki usiishie tu kupenda bali nenda hatua moja ya ziada ambayo ni kufanya ili upate unachopenda
Soma zaidi hapa; Matendo hutibu huoga
Yawezekana kuna sababu zinazokuzia kufanya unachotaka, au kuna vitu ambavyo wewe unasingizia na kuvibebelea na kuona kama sababu ya wewe kutofanya. Ziweke chini sababu zote na anza kufanya kidogo ili upate mafanikio makubwa mbeleni kwani dawa ya moto ni moto na haba na haba hujaza kibaba.
Anza sasa.
Wakati ni sasa
Muda ni sasa
Badilika sasa
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA