Kuwa Na Sababu


Kila kitu ambacho kipo lazima kuna sababu ya kitu kile kuwepo na kitu chochote ambacho kinafanyika lazima kuna sababu ya kitu kile kufanyika.
Lazima kuna sababu ya wewe kufanya kitu kile ambacho unafanya sasa hivi. Kama unanona unafanya kitu bila ya kuwa na sababu basi nakushauri acha kufanya sasa na anza tena
Acha ili uweke mpango wa kufanya kitu hicho. Lazima ufanye kitu  chochote ukiwa na sababu ya kufanya kitu hicho. 
Soma  zaidi hapa, Anza Na Moja
Usitembee katika dunia hii bila ya kuwa na wazo kubwa sana. Kuwa na wa,o kubwa la kufanya kitu hadi wale watakaoliona waogope.

 Wazo lako linahitaji moja kati ya vipengele vifuatavyo.

1. Wazo la kutoa huduma kwa watu ili wafaidike na huduma yako kubwa

2. kupunguza bei ya bidhaa za watu ambazo wanazipata ili wapate huduma kwa bei rahisi lakini yenye kiwango cha juu

3. wazo la kuwafanya watu wenye wafurahie mazingira yao ya kazi au wafurahie maisha kujumla

Kama wazo na mpango  wako haujagusa moja kati ya vipengele hivyo hapo juu. Kaa tena  uufikirie mara ya pili

Basi baada ya hapo nina hakika utakuwa na sababu ya kufanya kitu hicho na sababu ya kitu chochote huwa anaijua mtengenezaji wa kitu hicho. Mtengenezaji wa mfagio ndiye anayejua sababu ya kwa nini alitengeneza mfagio huo.
Sasa najua utakuwa na sababu ya kufanya kile ambacho unakifanya. ndio lazima sababu ya kufanya kitu hicho ipo

Kitu kingine ambacho unahitaji kuwa nacho ni msukumo wa ndani. Msukumo wa ndani utakufanya uweze kufanya  kazi kwa bidii. Kumbe usifanye kazi kwa sababu umefanya bali fanya kwa sababu una sababu ya kufanya hivyo na msukumo wa ndani.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X