Mambo muhimu kuhusu muda.




Kwa siku mwanadamu ana masaaa 24. Wengine wanyatumia masaa 24 kufanya mambo makubwa wakati wengine wanafanya mambo ya kawaida sana (mambi ya mazoea). Wakati unahangaika kufanya jambo fulani hakuna anayejihangaisha na wewe lakini ukishafanikisha wataanza kijitokeza watu na kuanza kuonesha kupendezwa na kile unachofanya.
Watu wanachoangalia   ni je, wewe umeweza kufanya? Je kazi muhimu umeweza kuifanya? Kumbe wakati unafanya kazi yeyote unahitaji kuyafahamu yafuatayo;
1.       Anza kufanya kazi yenye umuhimu mkubwa sana kwako.
Lazima unapoamka asubuhi unaanza kwa kuandika  mambo ambayo utayafanya ndani ya siku husika. Anza kufanya kazi yenye umuhimu mkubwa sana.
Brian Trancy katika kitabu chake cha eat that frog anasema
kitu cha kwanza kufanya unapoamka asubuhi ni kumla chura mzima”. Kama kuna kazi ya kufanya ndani ya siku husika anza kwa kufanya kazi ngumu sana, kazi ambayo inakutisha. Kazi ambayo inakuletea mafanikio asilimia 80%. Ifanye kazi hiyo mpaka pale itakapokuwa imeisha. Usiache kufanya kazi hiyo kwa sababu yoyote. Kama litajitokeza jambo la kufanya ndani ya muda wa kazi yako liweke pembeni na ulifanye baadae.
2.       Huwezi kusimamia muda labda tu unaweza kujisimamia mwenyewe. Kwa hiyo tunapozungumzia kuhusu kusimamia muda tunakuwa tunazungumzia kuhusu kusimamia maisha binafsi.
3.       Huwezi kuweka akiba ya muda. Labda unaweza kuutumia muda kufanya kazi zako mbalimbali. Muda hauwezi kuwekwa akiba kwa sababu unakimbia kwa kasi kubwa sana.
Kitu kingine unachoweza kufanya ndani ya muda wako ni kwamba acha kufanya mambo madogo madogo ndani ya muda wako. Anza kufanya mambo yenye thamani kubwa sana.
Kabla ya kufanya kitu jiulize kinaleta nini kwenye utendaji wako, kinaleta nini kwenye maisha yako?
·         Kama hakina maanakubwa achana nacho
·         Kama kina maana kubwa sana endana nacho.
http://www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X